Breaking News

CHAMA CHA WASAMBAZAJI WA FILAMU NA SHIRIKISHO LA FILAMU TANZANIA (TAFF), WAMEPONGEZA WAZIRI NAPE NNAUYE

Mwenyekiti wa Chama cha Wasambazaji wa Filamu nchini, Moses Mwanyilu,akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam mapema leo kuhusu kuipongeza serikali kupitia wizara husika katika kuanzisha oparesheni ya kuwakamata walanguzi wa kazi za wasanii nchini.
Rais wa Shirikisho la Filamu Tanzania (TAFF) Simon Mwakifamba akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani).
Katibu wa Chama cha Wasambaji wa Filamu Tanzania, Suleiman Ling'ande, akifafanua jambo katika mkutano huo.
Waandishi wa habari wakimsikiliza mwenyekiti wa chama cha wasambaji wa filamu nchini,Moses Mwanyilu (hayupo pichani) wakati akizungumza nao kuhusu wizi wa ulanguzi wa kazi za wasanii nchini.

Na Frank Wandiba;
Chama cha Wasambazaji wa  Filamu Tanzania  na Shirikisho la Filamu Tanzania (TAFF) wamepongeza hatua za makusudi zinazochukuliwa na Waziri wa Habari,Utamaduni,Sanaa na Michezo Mhe, Nape Nnauye za kuhakikisha anatokomeza mtandao wa waharamia na wauzaji wa kazi za wasanii bila kufuata utaratibu za kisheria nchini.

Pongezi hizo zimetolewa mapema leo jijini Dar es salaam Mwenyekiti wa chama cha wasambazaji wa filamu nchini Bw, Moses Mwanyilu kufatia hatua zinazochuliwa na serikali sasa kuwa zimekuja muda muafaka kwani ndio kilio chao cha muda mrefu kutokana na baadhi ya wafanyabiashara na wasambaji wa kazi za wasanii filamu na muziki za kutoka  ndani na nje ya nchi ambao sio waaminifu kuiingiza na kuuza bidhaa hizo bila ya kufuata utaratibu wa sheria jambo linalopelekea kuikosesha serikali mapato.

Amesema wafanyabiashara hao ambao sio waaminifu wamekuwa wakidurufu kazi za wasanii wa filamu za ndani na kuziingiza sokoni hatua ambayo inapelekea wasanii kushindwa kunufaika na kazi zao kwani uziuza kwa bei ya chini jambo ambalo linasababisha soko la filamu za ndani kudidimia.

Aidha bw, Mwanyilu ameongeza kuwa  baada ya kilio cha muda mrefu hatimaye serikali kupitia kwa wizara inayohusika na masuala ya sanaa imeanza kuchukua hatua za makusudi kutatua tatizo hilo kwa kuanza kufanya oparesheni ya nguvu ya kukamata walanguzi wa kazi za wasanii nchini katika maeneo ya kariakoo.

“Kwa niaba ya chama cha wasambazaji wa filamu na shirikisho la filamu Tanzania pamoja na vyama vyote vya shirikisho wanapenda kutoa shukrani za dhati kwa wizara ya habari kupitia waziri wake,Mhe Nape Nnauye na wadau wengine ikiwemo mamlaka ya mapato Tanzania (TRA), Bodi ya filamu,Cosota na Baraza la Sanaa Tanzania kwa hatua walizoanza kuchukua kuhakikisha kazi za wasanii zinauzwa kwa kufuata utaratibu uliowekwa na unaotambulika”

Nae  Katibu wa chama cha Wasambaji wa Filamu Tanzania, bw Suleiman Ling’ande amesema tatizo la uharamia katika kazi za wasanii nchini limekuwa ni changamoto ya muda mrefu kufuatia kuwepo na sheria ambayo imekuwa ikishindwa kuwabana wahusika hao kwa kutoa adhabu kali zaidi ili kazi za wasanii ziweze kuwanufaisha wasanii pamoja na kuliongezea kipato taifa kwa kulipa kodi.

Kwa upande wake Rais wa Shirikisho la Filamu Tanzania (TAFF),Bw Simon Mwakifamba amesema anaunga mkono hatua zinazoendelea kuchukuliwa na serikali pamoja na wadau wengine za kuhakikisha wanatokomeza uharamia wa kazi za wasanii nchini kitu kinachowaongezea motisha waigizaji hao kuendelea kutengeneza kazi nzuri za kuelimisha jamii.