WASANII KUNUFAIKA NA MFUMO MPYA WA UONYESHWAJI FILAMU
Msemaji kutoka kituo cha Sibuka Televisheni wa
kwanza kulia Bw. George Nangale akiongea na waandishi wa habari (hawapo pichani)
wakati wa uzinduzi wa kipindi cha INABAMBA “Ni bongo movie bandika bandua”
kitachokuwa kinaonyeshwa katika kituo hiko cha matangazo uliofanyika leo jijini
Dar es salaam, kushoto ni Afisa habari wa kampuni ya Step Entertainment
Bw. Moses Mwanyilu
Afisa habari wa kampuni ya Step Entertainment Bw.
Moses Mwanyilu wa kwanza kushoto akiongea na waandishi wa (habari hawapo
pichani) wakati wa uzinduzi wa kipindi cha INABAMBA “Ni bongo movie bandika
bandua” kitachokuwa kinaonyeshwa katika kituo cha matangazo Sibuka Televisheni
uliofanyika leo jijini Dar es salaam,katikati ni , Msemaji kutoka kituo cha
Sibuka Televisheni Bw. George Nangale na wa kwanza kushoto ni Mkurugenzi Masoko
kutoka Startimes Bw. Awino Felia.
WASANII wa Filamu nchini wanatarajia kunufaika na kazi zao kufutia
makubiliano ya Kampuni ya Star Media Tanzania Ltd (Startimes), pamoja na Steps
Entertainment za kutumia kazi zao kwenye vituo vya televisheni nchini.
Akizungumza waandishi wa habari leo, Mkurugenzi Mtendaji wa
Sibuka Media, Dkt. George Nangale alisema kazi hiyo itafanywa kwa
ushirikiano na taasisi hizo ili kuweza kuwasaidia wasanii kunufaika na kazi zao
kupitia luninga badala ya kuwasubiri wateja wao kuzinunua katika santuri
(DvD).
“Tumefikia uamuzi huu baada ya kuona ombwe lililopo sasa katika
kuzifikisha filamu zetu kwa walio wengi pamoja na kwamba Watanzania wana mwamko
mkubwa wa kuzitazama filamu hizi zenye mafunzo ya maisha na burudani”
alisisitiza Mkurugenzi huyo.
Kwa upande wake Msanii wa Bongo Movie, Mwanaheri Hamad alisema
uonyeshaji wa kazi zao katika vituo vya televisheni utawanufaisha wasanii
chipukizi ambao kazi zao bado hazijaonekana.
Amesema kuwa kutokana na mkataba huo wa kurusha filamu hzo umerahisisha
soko za kazi hizo katika mfumo DvD ambapo ulikuwa unatumiwa hapo awali.
Filamu hizo zitaonyeshwa kupitia king’amuzi cha StarTimes chaneli
111 ikijulikana kama Sibuka Maisha Steps chaneli kila siku na itaanza
kuonyeshwa Ijumaa hii tarehe 29 Julai, 2016.



