Breaking News

WAZIRI MKUU MGENI RASMI KONGAMANO LA USHIRIKI WA WATANZANIA KATIKA UWEKEZAJI.

Katibu Mtendaji Baraza la Taifa la Uwezeshaji wananchi kiuchumi Bi.Bengi Issa akifafanua jambo kwa waandishi wa habari na kuwahimiza watanzania kushiriki kikamilifu katika kongamano la siku mbili la ushiriki wa watanzania katika uwekezaji ili kuiwezesha serikali kuweka mipango madhubuti ya kuhakikisha waanchi wake wanashiriki kikamilifu katika uchumi wa nchi yao
Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera na Uratibu), Dk.Hamis Mwinyimvua (kulia) akizungumza na wandishi wa habari (hawapo pichani) kuhusu kongamano la siku mbili la ushiriki wa watanzania katika uwekezaji ili kuiwezesha serikali kuweka mipango madhubuti ya kuhakikisha waanchi wake wanashiriki kikamilifu katika uchumi wa nchi yao.Kulia kwake ni Katibu Mtendaji Baraza la Taifa la uwezeshaji wananchi kiuchumi Bi.Bengi Issa.

Picha na Daudi Manongi, MAELEZO

SERIKALI kupitia Ofisi ya Waziri Mkuu imeandaa kongamano kongamano la siku mbili la uwekezaji litakalojadili mipango madhubuti ya kuhakikisha Watanzania wanashiriki kikamilifu katika ujenzi wa uchumi wa nchi yao.

Kongamano hilo linatarajia kufanyika katika ukumbi wa Benki Kuu Jijini Dar es Salaam kuanzia tarehe 21 -22 Julai mwaka huu.

Hayo yamesemwa leo Jijiji Dar es Salaam na Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera na Uratibu) Dkt.Hamis Issa wakati wa mkutano wake na waandishi wa habari kuhusu kongamano hilo.

Dkt. Issa alisema Serikali imepitisha Sera ya ushiriki wa watanzania katika sekta ya Mafuta na Gesi asilia, hatua ambayo itasadia wananchi wazawa kushiriki kikamilifu katika ujenzi wa uchumi wa nchi yao.

 “Msukumo mkubwa wa serikali kwa sasa ni kuongeza ushiriki katika  uwekezaji unaochochewa na ugunduzi mkubwa wa gesi asilia katika kina kirefu cha bahari  ambao utaweza  kuwanufasha Watanzania” alisema Dkt. Issa.

Aidha alisema kuwa kutokana ushiriki huo wa Watanzania kuwa suala mtambuka na agenda endelevu, Serikali iliiagiza Baraza la Taifa la Uwezeshaji kuanzisha Idara ya ushiriki wa watanzania katika uwekezaji ambayo imeanza kutekeleza majukumu yake mwezi Novemba mwaka 2015.