DART NA MAXCOM WAZINDUA HUDUMA YA KUWEKA SALIO KATIKA KADI ZA MABASI YA MWENDO WA HARAKA KUPITIA MAWAKALA WA MAXMALIPO
Msemaji wa Kampuni ya Mabasi ya
Mwendo wa haraka jijini Dar es Salaam (kushoto) Bw. Deus Bugaywa akisisitiza
jambo kwa waandishi wa habari (hawapo pichani) wakati wa uzinduzi wa mfumo wa
kuweka salio katika kadi za mabasi ya mwendo wa haraka kupitia kwa mawakala wa MaxMalipo mapema hii
leo jijini Dar es Salaam, Katikati ni Afisa Mwendeshaji Mkuu wa Kampuni ya
Maxcom Africa Ltd. Bw. Ahmed Lussasi na mwisho kulia ni Mkuu wa Kitengo cha
Biashara toka Maxmalipo Bw. Deogratius Lazari.
Mkuu wa Kitengo cha Biashara toka
Maxmalipo Bw. Deogratius Lazari akionesha kwa waandishi wa habari (hawapo
pichani) namna ya kufanya malipo wakati
wa uzinduzi wa mfumo wa kuweka salio katika kadi za mabasi ya mwendo wa haraka kupitia kwa mawakala wa MaxMalipo mapema hii
leo jijini Dar es Salaam, kushoto ni Afisa Mwendeshaji Mkuu wa Kampuni ya
Maxcom Africa Ltd. Bw. Ahmed Lussasi.
Afisa Mwendeshaji Mkuu wa Kampuni
ya Maxcom Africa Ltd. Bw. Ahmed Lussasi akionesha moja ya kadi za mabasi ya
mwendo wa haraka wakati wa uzinduzi wa mfumo wa kuweka salio katika kadi za
mabasi ya mwendo wa haraka kupitia kwa
mawakala wa MaxMalipo mapema hii leo jijini Dar es Salaam, kulia ni Mkuu wa
Kitengo cha Biashara toka Maxmalipo Bw. Deogratius Lazari.
Baadhi ya waandishi wa habari
wakimfuatilia kwa makini Mkuu wa Kitengo cha Biashara toka Maxmalipo Bw.
Deogratius Lazari namna ya kuongeza salio kwenye kadi za mabasi ya mwendo wa
haraka wakati wa uzinduzi wa mfumo wa kuweka salio katika kadi za mabasi ya
mwendo wa haraka kupitia kwa mawakala wa
MaxMalipo mapema hii leo jijini Dar es Salaam.Picha zote na Eliphace Marwa -
Maelezo
*******************
Kampuni
ya Maxcom Africa – Maxmalipo kwa kushirikiana na Kampuni ya Mabasi
yaendayo Haraka wamezindua rasmi Mfumo unaowezesha watumiaji wa Usafiri wa Mwendo
haraka (mwendo Kasi) kuweka salio katika kadi za usafiri kupitia kwa Mawakala
wa Maxmalipo popote hapa nchini.
Hivyo
kuanzia sasa wasafiri wenye kadi maalumu za Usafiri (Dart card) wanaweza kufika
kwa wakala yeyote wa Maxmalipo kisha atampatia fedha taslimu yenye thamani na
salio analohitaji kuweka ndani ya kadi yake na Wakala atamukea salio ambalo
litamwezesha kusafiri katika mabasi ya mwendo haraka kwa kutumia kadi yake
hiyo.
Akiongea
kwenye uzinduzi huu Afisa Mwendesgaji mkuu wa Maxmalipo Bw. Ahmed Lussasi
Amesema kuwa kampuni ya Maxcom imekuwa msatari wa mbele katia kujenga
mifumo imara ya kieletroniki inayorahisisha ukusanyaji wa mapoato.
“
Lengo kubwa la kampuni ya Maxcom Africa ni kujenga na kutengeneza mifumo imara
na madhubuti ambayo inalenga kurahisisha ukusanyaji wa mapato kwa njia ya
kielektroniki pia kusimamia na kudhibiti mianya ya upotevu wa mapato kwa
kutumia mifumo ya Kielektroniki,” alisema Bw. Lussasi.
Naye
Msemaji wa Kampuni ya Mabasi yaendayo Haraka Bw. Deus Bugaywa aliongeza kuwa
Maxmalipo ikishirikiana na Uongozi wa mradi wa mabasi ya mwendo haraka wamekua
mstari wa mbele katika kufanya uvumbuzi wa njia mbalimbali za kiteknolojia
zitakazo warahisishia wasafiri pamoja na watumiaji wa mabasi haya kuendelea
kujipatia huduma kwa urahisi zaidi bila usumbufu wowote.
“Naweza
kuwadhihirishia kwa ushirikiano huu tulionao na Maxmalipo katika mradi huu
umeleta mageuzi makubwa katika sekta ya usafirishaji nchini kwetu, barani
Afrika na duniani kwa ujumla,” alisema Bw. Bugaywa.
Naye
Mkuu wa Kitengo cha biashara katika kampuni ya Maxmalipo Bw. Deogratius Lazari,
amesema kuwa Maxcom Africa ina Zaidi ya mawakala 15000 nchi nzima ambao
wamewezeshwa kutoa huduma hii kwa watumiaji wa kadi hizi za mwendo haraka.
“Mawakala
hawa wa Maxmalipo wapo jirani na makazi ya watu hivyo wasafiri wanaweza
kujipatia huduma hii kabla ya kufika kwenye vituo vya mabasi ya mwendo haraka
na kupunguza foleni za abiria kwenye vituo vya mabasi ya hasa wale wanaokua
wakihitaji kuweka salio kwenye kadi zao,” alisema Bw. Lazari.
Maxcom
Africa imekua ni Moja ya Kampuni za Kitanzania iliyofanikiwa katika uwekaji wa
mifumo madhubuti ya ukusanyaji na usimamizi wa mapato hapa Tanzania hasa katika
miradi mikubwa ikiwamo huu wa mabasi ya Mwendo Kasi, TRA, Vivuko, Mahospitali
(Moi) na kwenye Kodi za halmashauri.






