Aliyetajwa Kufariki Katika Ajali Ya Ndege Arusha,.. Akutwa Yupo Hai
Mfanyakazi Wa Hoteli Za Kitalii Za Andbeyond Serengeti, Moses Muhina Aliyetajwa Kuwa Ni Miongoni Mwa Abiria Waliofariki Dunia Katika Ajali Ya Ndege Ya Shirika La Coastal Aviation, Imebainika Alibadili Ndege Muda Mfupi Kabla Ya Safari Ili Kuwahi Kazini.
Muhina Ambaye Ni Mwongozaji
Watalii Katika Hoteli Hiyo, Alikuwa Aondoke Na Ndege Ya Coastal Aviation Saa
Nne Asubuhi Lakini Viongozi Wa Hoteli Walimbadilishia Ndege, Hivyo Aliondoka Na
Air Exel Iliyofika Salama Serengeti.
Akizungumza Na Gazeti Hili,
Meneja Uendeshaji Wa Hoteli Ya Andbeyond Serengeti Under Canvas, Mussa Matala Alisema
Muhina Ambaye Anasomeka Kwenye Orodha Ya Ndege Kama Maina Alikuwa Apande Ndege
Hiyo Lakini Walimbadilishia.
Alisema Waliomba Aondolewe
Kwenye Orodha Ya Wasafiri Wa Ndege Hiyo Lakini Kwa Bahati Mbaya Hadi Ndege
Ilipoondoka Jina Lake Lilikuwapo.
Wakati Huohuo, Raia Watano
Wa Kigeni Ambao Walifariki Dunia Katika Ajali Hiyo, Akiwamo Rubani Dewald
Raubenheimer Raia Wa Afrika Kusini, Ambaye Kwenye Orodha Ya Awali Ya
Waliofariki Jina Lake Halikuwapo Anatarajiwa Kusafirishwa Leo.
Mhudumu Wa Chumba Cha
Kuhifadhi Maiti Katika Hospitali Ya Mkoa Ya Mount Meru, Francis Costa Alisema
Miili Mitatu Kati Ya 11 Imechukuliwa Na Ndugu Zao.
Alisema Miili Iliyochukuliwa
Ni Ya Ndugu Wawili Waliokuwa Wakurugenzi Wa Masai Wondering, Nasibu Na Shatri
Mfinanga.
Mwingine Ni Wa Joyce Mkama Ambaye
Alikuwa Mfanyakazi Wa Hoteli Ya Serena.
“Uchunguzi Wa Miili Ya
Wageni Kutoka Nje Ya Nchi Unaendelea Na Ukikamilika Itasafirishwa Kwa Mazishi
Katika Nchi Za Afrika Kusini, Ujerumani Na Italia,” Alisema.
Ndege Hiyo Namba 5H-EGG Aina
Ya Cessna Grand Caravan Ilianguka Baada Ya Kugonga Kingo Za Creta Ya Empakai,
Umbali Wa Mita 3,250 Kutoka Usawa Wa Bahari Ikitoka Kilimanjaro Kwenda Hifadhi Ya
Serengeti.
Kamanda Wa Polisi Mkoa Wa Arusha,
Charles Mkumbo Alisema Uchunguzi Unaendelea Kuhusu Ajali Hiyo.
Imeandikwa Na Mussa Juma,Mwananchi



