Startimes Yazindua Ofa Ya Mfalme Wa Familia
Meneja
Uhusiano na Masoko wa kampuni hiyo Juma Suluhu.
KAMPUNI ya Star Media
(T) Ltd kupitia chapa yake ya StarTimes katika msimu huu wa Sikukuu imekuja na
Ofa ya aina yake ijulikanayo kama ‘Mfalme wa Familia’ kwa ajili ya wateja
watakaopenda kujiunga na huduma za kampuni hiyo.
Hayo yamebainishwa jijini Dar es Salaam
na Meneja Uhusiano na Masoko wa kampuni hiyo Juma Suluhu akizungumza na
waandishi wa habari, amesema StarTimes inatambua umuhimu na uzito wa
kipindi hiki cha sikukuu kwa watanzania hivyo wamejipanga vyema kutoa burudani
ya kiwango cha hali ya juu.
“Tumewaletea watanzania Ofa
tuliyoipatia jina la ‘Mfalme wa Familia’, tumeiita hivyo kwa sababu sisi ni
wafalme wa Burudani za Familia, ukianzia filamu, michezo kama mpira wa miguu,
kikapu, katuni, Muziki, Ndondi na vingine vingi. Tuna vipindi ambavyo watoa
huduma wengi hawana, hivyo ni fursa ya kipekee kwa watanzania kufurahia,”
amesema Juma.
Aidha ameongeza kuwa ofa hiyo inaenda
sambamba na kushuka bei ya king’amuzi cha Antenna ambacho awali kilikuwa
kikiuzwa kwa Tsh 47,000 ambacho kwa wakati hua kitapatikana kwa bei ya punguzo
ya sh. 34,000 .
“Ofa yetu ina mambo makubwa matatu,
Jambo la kwanza ni hilo punguzo la bei ya king’amuzi cha Antenna, pili ni
king’amuzi cha Combo ambacho kinatumia dish na Antenna ambacho awali kilikuwa
kikiuzwa kwa Tsh 86,000 sasa kitapatikana kwa Tsh 78,000 huku mteja
atakayenunua atapata kifurushi cha Mwezi mzima pamoja na Dish Bure”, amesema
Juma.
“Tatu ni luninga zetu za kidigitali,
hapa unapata vitu vitatu, cha kwanza luninga zetu zina king’amuzi ndani, cha
pili ukinunua luninga yetu unapatiwa dish bure na cha mwisho utaunganishwa
kifurushi cha Uhuru kwa mwezi mmoja Bure”, ameongeza.
Licha ya ofa hizo wateja wa StarTimes
wataweza kupata Chaneli zote za Kifurushi cha Kili katika kifurushi cha Uhuru
kuanzia Disemba 1, 2017 ikiwa ni sehemu ya Promosheni ya Mfalme wa Familia
ambayo imeletwa na StarTimes Tanzania.




