POLISI: Mnunuzi Wa Nyumba Za LUGUMI Alitumwa Na LUGUMI Mwenyewe

Dk. Louis Shika
Jeshi la Polisi Kanda Maalum ya Dar
es Salaam limesema kuwa Dk. Louis Shika ambaye alishinda mnada wa ununuzi wa
nyumba za Said Lugumi na baadae kuzua kizaa-zaa, alitumwa na Lugumi mwenyewe.
Dk. Louis ambaye alifunga mnada wa nyumba hizo
kwa kuahidi kulipia shilingi milioni 900, alishindwa hata kutoa robo ya kiasi
hicho kwa mujibu wa masharti ya mnada hali iliyopelekea kufikishwa katika kituo
cha polisi.
Kamanda wa Jeshi la Polisi wa kanda hiyo,
Lazaro Mambosasa amesema kuwa jeshi hilo linahisi kuwa alitumwa na Lugumi
kutokana na mazingira ya tukio husika.
“Aliwekwa na Lugumi ili kukwamisha mnada,”
Mambosasa anakaririwa na Mwananchi ingawa aliweka angalizo kuwa hana vielelezo
kuhusu hilo.
“Ingawa sina facts (vielelezo) kuthibitisha
hilo, lakini alichokuwa anafanya kinatufanya tuamini hivyo. Kwasababu alikuwa
anapandisha bei kila nyumba ili washiriki wengine wasinunue,” aliongeza.



