TAMWA KUAZIMISHA SIKU 16 ZA KUPINGA UKATILI WA KIJINSIA

Mkurugenzi Mtendaji Wa Tamwa Bi Edda Sanga
Na Sala Mlawasi
Chama cha waandishi wa wahabari wanawake Tanzania (TAMWA), kinaungana na mashirika mengine yanayopinga ukatili Wa kijinsia na kutetea haki za binadamu kuzindua maadhimisho ya siku 16 za kupinga ukatili Wa kijinsia.
Chama cha waandishi wa wahabari wanawake Tanzania (TAMWA), kinaungana na mashirika mengine yanayopinga ukatili Wa kijinsia na kutetea haki za binadamu kuzindua maadhimisho ya siku 16 za kupinga ukatili Wa kijinsia.
Akizungumza jijini Dar es salaam, Mkurugenzi Mtendaji Wa
Tamwa bi Edda Sanga alisema maadhimisho hayo ambayo yanaanza November 25 na
kufikia kilele 10 December yatajikita zaidi katika kutoa Elimu zaidi juu ya
athari za ukatikli wa kijinsia kwa ndugu jamaa na marafiki pamoja na wazazi kwa
kushirikiana na serikali kuvitokomeza vitendo hivyo vya ukatili Wa
kijinsia kwa wanawake na hasa watoto Wa kike ambao wako chini ya umri Wa miaka
18.
Alisema kupitia kitengo chake cha Usuluhisho cha CRC
kuonyesha kuwa vitendo vya ukatili Wa kijinsia hasa ubakaji vimeongezeka katika
kipindi cha miezi Nane kuanzia mwezi January hadi Augusti mwaka 2016, kesi
zilizoripotiwa katika kituo cha Amana ni 9, wakati wa kipindi cha mwaka huu
2017 jumla ya vitendo vya Unyanyasaji vimeongezeka hadi kufikia 57.
"tathimini ya utendaji kazi wa kituo cha hospitali ya
Amana jijini dar es salaam imeonesha kiwango cha ubakaji kwa mwaka huu ziko juu
idadi ya watoto 141 walio chini ya umri wa miaka 18 ukilinganisha na idadi ya
watu wazima 27 na hii ni kwa wale wanaotoa taarifa hivyo wanaimani idadi ni
kubwa zaidi kwa wasiotoa taarifa" Alisema Bi sanga .
Aidha Bi Sanga ametoa wito kwa wanajamii na serikali kwa
ujumla kwani kujikita zaidi katika kuweka pamoja na kutoa elimu kwa jamii
juu ya athari za ukatili wa kijinsia na swala la walinzi wa watoto ni swala la
jamii yote kwa ujumla .
Kwa upande wake mwakilishi wa jeshi la polisi kutoka kituo
cha polisi wa kata ya kivule Wilaya ya ukonga Bw kenedi Nyaikoba alisema ipo
haja ya kujijita zaidi katika kutoa elimu kwa jamii watu wengi hawajui ukatili
nini ni ila wakielimishwa wimbi kubwa la ukatili wa kijinsia utapungua .
Pia Bw Nyaikoba pamoja na uchache wa utendaji wa swala la
kupunguza ukatili wa kijinsia kata ya kivule umepungua sana kwani zamani
walikua wanakeketa watoto wakike ila kwa sasa limekwisha.



