Afariki Dunia Baada Ya Kuanguka toka Ghorofa Ya 62

Raia mmoja wa China, Wu Yongning
anayependelea kuparamia na kuruka katika majengo marefu kutoka jengo moja
kwenda jingine amefariki dunia baada ya kukosea hatua wakati akifanya kile
anachopenda kufanya katika maghorofa.
Kijana huyo anayeparamia majengo
makubwa bila ya vifaa vyovyote vya usalama hujirikodi video huku akishikilia
mkono mmoja akining'inia kutoka juu ya mjengo hayo kwa vidole vyake tu vya
mkononi.
Kilichofuata baada ya hapo ni jambo
la kushtusha na la kusikitisha kwani raia huyo alianguka kutoka katika ghorofa
ya 62 kutoka juu na kufariki papo hapo.
Kwa mujibu wa shirika la habari
la Uingereza (BBC) maelfu ya wafuasi wake walishikwa na wasiwasi alipoacha
kuweka video za vituko vyake katika mitandao kama vile Huoshan na Kuaishou,
lakini kifo chake kilithibitishwa katika siku chache, kwanza na mpenzi wake
baadaye likafuata tangzo la maafisa wa polisi.
Video ya kushtusha ya kilichoonekana
kuwa muda wake wa mwisho wa uhai wake akiwa katika hekaheka za kuparamia kuta
za majengo marefu katika mji wa Changsha city ilianza kusambaa katika mtandao
wiki hii.
Kifo chake kimezusha maswali mengi ya
wasiwasi na ya kutafakari pamoja na mijadala mizito kuhusu kuhatarisha maisha
katika kutafuta pesa.



