Msichana Aliyebakwa Na Walimu Wawili Kwa Wiki 3 Hoi Hospitali

Msichana
wa India ambaye alidaiwa kubakwa na walimu wawili wa shule katika kipindi cha
wiki tatu yuko katika hali mahututi baada ya kulazimishwa kutoa mimba.
Madaktari
wameiambia BBC idhaa ya Hindi kuwa ubongo wake umeharibika.
Polisi
imemtia nguvuni Mkuu wa shule yake na mwalimu wake katika jimbo la kaskazini
mwa India la Rajasthan.
Polisi
wanasema kuwa alipoteza fahamu baada ya washukiwa kumlazimisha kutoa mimba
katika hospitali ya kibinafsi.
Polisi
pia wanachunguza nafasi ya hospitali katika tukio hilo.
Msichana
huyo mwenye umri wa miaka 18 alilazwa hospitalini baada ya kuhisi maumivu
makali ya tumbo na wahudumu katika shule yake wakabaini kwamba alikuwa
mjamzito.
Hali yake
ya afya ilianza kuwa mbaya kwa haraka baada ya kuavia mimba, lakini haijafahamika
wazi ni nini hasa kilichoifanya hali yake kuwa mbaya,alisema polisi katika
wilaya ya Sikar said.
Shule
hiyo iliyopo wilaya ya Sikar, imefungwa kwa sasa na mamlaka katika eneo hilo.
Polisi
wanaamini kuwa masomo ya ziada yanayotolewa katika saa ambazo si za kawaida
yalitumiwa kuwaita wanafunzi ili kuwezesha vitendo kama hivyo vya unyanyasaji
kufanyika.
Bado
polisi hawajaweza kurekodi taarifa kutoka kwa muathirika.
"Hili
ni tatizo baya na hatua kali zitachukuliwa dhidi ya wahusika ,"alisema
afisa wa polisi Kushal Singh.
Chanzo-
BBC



