Jamaa Apewa Kichapo Na Kundi La Wanawake.. Baada Ya Kurudi Na Mchepuko Na Kumtaka Mkewe Apishe Kitandani

Picha haihusiani na habari hapa chini
Kundi la wanawake katika Mtaa Majengo wilayani Kahama mkoani
Shinyanga wamemshambulia kwa kumpiga mkazi wa mtaa huo aliyefahamika kwa jina
la Andrew baada ya kwenda na mwanamke mwingine nyumbani kwake na kumtaka mke wake
awapishe kitandani ili walale.
Tukio
hilo limetokea usiku wa kuamkia leo ambapo majirani hao walifikia hatua hiyo
baada ya kuamshwa na kelele zilizokuwa zikiendelea baina ya wanandoa hao.
Akizungumza
na Kahama fm, Mke wa mwanaume huyo, Mariam Abdallah, (32) amesema mume wake
alifika usiku majira ya saa tano akiwa na mwanamke huyo ambapo alimtaka
awapishe kitandani ili walale na yeye akalale sebuleni.
Hata
hivyo baada ya kuona hivyo walianza malumbano ndipo majirani walipofika na
kuanza kumshambulia mume wake wakisema amewadharirisha wanawake wa eneo hilo.
Kwa
upande wake mume wa Mke huyo bwana Andrew amesema mwanamke huyo ni mke wake wa
pili, na kwamba alifika nyumbani kwa lengo la kujiandaa kwenda kumpokea mama
yake mzazi aliyekuwa anatoka Dar es Salaam ambapo wangeenda wote watatu kwa
kuwa alishawatambulisha.
Kwa
upande wake mkuu wa kitengo cha dawati la jinsia na watoto kutoka jeshi la
Polisi wilayani Kahama, Gumba Mipawa amethibitisha kutokea tukiko hilo na
kwamba wanaendelea kuwahoji wanandoa hao.
Kwa
mujibu wa kitengo cha dawati la jinsia wilayani humo, hilo ni tukio la kwanza
kuripotiwa kwenye kitengo hicho tangu kianzishwe wilayani humo.



