Mahakama Ya KATIBA Yalitaka Bunge Kumshtaki Rais

Mahakama ya Katiba nchini Afrika Kusini imebaini kwamba bunge
la nchi hiyo lilishindwa kutimiza wajibu wake kwa kushindwa kumuwajibisha rais
wa nchi hiyo Ndg. Jacob Zuma juu ya kesi iliyokuwa ikimkabili ya matumizi
mabaya ya fedha za umma.
Uamuzi huo wa Mahakama ya Katiba ukiongozwa na Jaji Chris
Jafta nchini humo umeainisha kwamba bunge hilo ni lazima lianze mchakato wa taratibu
za kumfungulia mashitaka ingawa haikuwa wazi kwamba mchakato huo utaweza
kumuondoa madarakani kwa kupigiwa kura.
Mahakama hiyo ilikuwa ikisikiliza kesi iliyofunguliwa
na kambi ya upinzani ambayo ilitaka bunge la nchi hiyo kuanza mchakato wa
kumshitaki Rais Zuma.
Rais Zuma anatuhumiwa kutumia fedha za umma kuendeleza makazi
yake binafsi.



