Mbunge Wa Cuf Aliyejiuzulu Na Kutangaza Kugombea Kupitia Ccm Atukanwa Na Wananchi
Aliyekuwa Mbunge Kinondoni (CUF),
Maulid Mtulia ambaye amehamia CCM ametangaza nia ya kugombea tena ubunge katika
jimbo hilo kwa tiketi ya chama hicho tawala.
Desemba 2 Mtulia alijiuzulu nafasi ya
ubunge, huku akisema amefikia uamuzi huo bila kushawishiwa mtu yeyote na
amebaini Serikali ya CCM inafanya kazi kubwa ya kutekeleza Ilani na imefanya
vizuri katika mambo mengi ambayo upinzani iliahidi kuyatekeleza.
Baada ya hatua hiyo, chama cha CUF
upande wa Profesa Ibrahim Lipumba kilitangaza kuwaomba radhi wapiga kura wa
Kinondoni kwa Mtulia kujiuzulu uanachama kisha ubunge.
Lakini jana Jumanne Desemba 19, 2017
kupitia andiko lake mtandaoni, Mtulia amesema atachukua fomu ya kuomba ridhaa
ya kuteuliwa ndani ya CCM ili agombee tena nafasi hiyo.
"Kwaza, nawasalimu wote na khasa
wananchi wenzangu wa jimbo la Kinondoni. Nawapa pole sana kwa maumivu makali
mliyoyapata kutokana na uamuzi wangu wa kujiuzulu ubunge wa jimbo letu la
Kinondoni kupitia chama cha CUF. Nawahakikishia kwamba bado nawapenda sana na
niko tayari kuwatumikia tena kwa lengo la kuleta Maendeleo kwenye jimbo
letu" aliandika Mtulia
Mtulia alitumia nafasi hiyo kutangaza
nia yake kutaka kugombea;"Nichukie fursa hii kutangaza nia kwa
wanakinondoni wote na Watanzania kwa ujumla kuwa nitachukua form ya kuomba
ridhaa kwenye chama changu cha CCM na endapo chama changu kitaridhia basi
nitakuja mbele yenu kuomba ridhaa ya kuwatumikia katika nafasi ya ubunge wa
jimbo letu Kinondoni"
Kufuatia ujumbe huo ndipo hapo baadhi
ya wananchi walianza kumpa maneno wakionyesha hisia zao juu ya jambo alilofanya
na analotaka kulifanya.
Baadhi ya Ujumbe na coment za wananchi===>>






