Kutoka Shinyanga: Muosha Magari Akatwa Masikio Baada Ya Kulawiti Mtoto Wa Miaka 3.

Kamanda wa jeshi
la polisi mkoa wa Shinyanga ACP Simon Haule akizungumza na waandishi wa habari
leo Disemba 21,2017.
Kijana aliyejulikana kwa
jina la Msigala Salum (24) amekatwa masikio yote mawili baada ya kumlawiti
mtoto mwenye umri wa miaka mitatu katika eneo la Majengo Mapya kata ya Lubaga
manispaa ya Shinyanga mkoani Shinyanga.
Tukio hilo limetokea Disemba
20,2017 majira ya saa tatu asubuhi ambapo kijana huyo anayejishughulisha na
shughuli ya kuosha magari mkazi wa Ndala alimdanganya mtoto huyo wakati
akicheza na wenzake nyumbani kwao.
Kwa mujibu wa mashuhuda wa
tukio hilo waliiambia Malunde1 blog kuwa kutokana na tukio hilo mtuhumiwa
alishambuliwa na wananchi kabla ya jeshi la polisi kufika eneo la tukio na
kumuokoa.
Akitoa taarifa kwa vyombo
vya habari leo Alhamis Desemba 21,2017 Kamanda wa Jeshi la Polisi mkoa wa
Shinyanga ACP Simon Haule alisema jeshi hilo linamshikilia Msigala Salum kwa
kosa la kulawiti mtoto huyo mwenye umri wa miaka mitatu ambaye tayari
amefanyiwa uchunguzi wa kidaktari.
Akielezea zaidi kuhusu tukio
kamanda Haule alisema mara baada ya tukio hilo baba mzazi wa mtoto alimkamata
mtuhumiwa na kumkata masikio yote mawili kwa kutumia kisu na kukimbia.
Source Malunde



