Naibu Meya Ilala Mhe. Kumbilamoto Awashukukia Wanaokwamisha Maendeleo Kisa Itikadi Za Vyama.
NAIBU
Meya wa Manispaa ya Ilala Na Diwani Wa Kata Ya Vingunguti Mhe Omary Kumbilamoto
amewaasa wananchi na watanzania kwa ujumla kuwa kamwe awataweza kupiga hatua na
kutatua changamoto mbalimbali zinazowakabili katika maeneo yao kama awataacha kuchanganya itikadi
zao za kisiasa katika mambo ya maendeleo.
Akizungumza katika mkutano wa
hadhara wa kusherekea kutumiza miaka miwili tangu kuchaguliwa kuiongoza kata hiyo alisema, maendeleo hayana chama wala itikadi ni ushirikiano kati ya viongozi na wananchi
wa eneo husika katika kubaini na kutatua kero zinazowakabili wananchi kwa
wakati.
"Nataka niwaeleze viongozi na wananchi
wa kata ya Vingunguti tuache kuendekeza siasa hususani katika mambo yanayohusu
maendeleo, siasa zinawekwe pembeni badala yake viongozi tujikite kuona namna
ambavyo tunaweza kutatua kero za wananchi hili kuwaletea maendeleo” Alisema Kumbilamoto.
Akizungumzia mafanikio na
changamoto katika kipindi cha miaka miwili tangu kuchaguliwa kuiongoza kata
hiyo alisema katika kipindi chake cha uongozi atajikita zaidi katika kuleta
mapinduzi makubwa katika Kata ya Vingunguti kwa kujikita katika kuboresha
sekta ya Afya, Miundominu Pamoja Na Kuwainua Vijana.
Mhe.Kumbilamoto alisema kumekuwepo na wanasiasa
wanapita kuwarubuni na kuwapotosha wananchi kuhusu changamoto ya ubovu wa
barabara ya Mnyamani hadi Vingunguti kuwa ameshindwa kuifanyia ukarabati jambo
ambalo si ukweli kuwa jukumu la kujenga Barababara limehahishwa kutoka kwa
halmashauri na kupelekwa kwa Wakala wa Ujenzi wa Barabara Mijini na Vijini TARURA.
Alisema amekuwa
akipokea vitisho na matusi hadi kufikia kutukanwa kwa mzazi wake kuhusiana na ubovu
wa Barabara hiyo jambo ambalo limekuwa likimuuma sana hivyo ameamua kutoa ufumbuzi juu ya changamoto hiyo ya barabara kuepukana na maswali hayo mengine yamekuwa yakihusisha na mgogaro wa kisiasa ulipo ndani ya Chama chake cha CUF.
“Natoa wito kwa wananchi
kuwapuuza wanasiasa ambao wamekuwa wakipita na kuwapotosha kwa mambo mbalimbali
likiwemo la ukarabati wa barabara ya Mnyamani hadi Vingunguti badala yake
wajikite zaidi katika kushirikiana na viongozi katika kutatua kero
zinazowakabili hili kusukuma gurudumu la
maendeleo” Alisema.
Aidha Mhe. Kumbilamoto aliongeza kuwa kama yeye ingekuwa ni kikwazo cha
kutokutengenezwa barabara hiyo angechuka hatua ya kujiuzuru ila kutokana
kutokuwepo chini yake na kutokuwa na jukumu hilo ameaaidi wananchi wa kata hiyo
kulifatilia kwa karibu mpaka litakalopatiwa ufumbuzi na ataendelea kuwatumikia
wananchi bila kujali itikadi zao za vyama wala ubaguzi.



