Breaking News

WAANDISHI WA HABARI WAPIGWA MSASA NAMNA VITUO VYA MKONO KWA MKONO (ONE STOP CENTER) VINAVYOENDESHA SHUGHULI ZAKE

Waandishi wa Habari kutoka media mbaliombali walioshiriki mafunzoya siku moja wakiwa katika picha ya pamoja.

Na Sala Mlawas
Jamii imeombwa kujitokeza kufungua vituo vya mkono kwa mkono yaani One Stop Center vitakavyotoa huduma za maswala ya ukatili wa kijinsia kwa wakati mmoja hivyo kusaidia  kupunguza mzunguko wa kupata ushahidi uliojitosheleza.

Kauli hiyo imetolewa jijini Dar es salaam na Afisa wa Polisi na Mratibu wa kituo cha One Stop Center kilichopo katika Hospitali ya Amana Bi. Christina Onyango wakati akiufungua mafunzo ya siku moja kwa waandishi wa habari yaliolenga kuwajengea uwelewa namna kituo hicho kinavyo endesha na kuratibu shughuli zake. 

Alisema kituo cha mkono kwa mkono kimekuwa msaada mkubwa katika kuwezesha kupatikanaji wa huduma zote kwa wakati mmoja kama vile Polisi, Hospitali, Huduma Za Ustawi Wa Jamii jambo ambalo limekuwa likisaidia kupunguza mzunguko kwa mhanga.

Aidha Bi Onyango aliongeza kuwa lengo kubwa la kufunguliwa kwa kituo hicho ni kutoa huduma stahiki ikiwemo kusaidia kupatikana ushahidi unaotakiwa na wenye kujitosheleza hivyo kupunguza mlundikano wa kesi za unyanyasaji, sambamba na mhanga kuweza kuhamishwa mahali anapoishi na kupelekwa sehemu usalama.

Bi Onyango amezitaja changamoto zinazowakabili kituo hicho kuwa ni ukosefu wa bajeti ambayo itatumika kuwezesha kugharamia gharama za ununuzi wa vitendea kazi kama vile mavazi ya wahanga na usafiri.

Pia Bi. Onyango alimalizia kwa  kusema kuwa baada ya kumsikiliza mhanga ambaye amefika na kutoa taarifa kisha utaratibu wa kuanza kufanya uchunguzi wa kujitosheleza uanza mara moja na pindi itakapobainika kweli uwepo kwa kosa muhusika atafikishwa katika vyombo vya sheria ili sheria ichukue mkondo wake.