MBOWE : Awashukia Wanaomshambulia Askofu KAKOBE

Mwenyekiti Wa CHADEMA Na Kiongozi Mkuu Wa Kambi
Rasmi Ya Upinzani Bungeni, Freeman Mbowe Amewataka Watanzania Kuwa Tayari
Kukosolewa Na Viongozi Wa Dini Kwani Ndiyo Wanaoliombea Taifa Liwe Na Amani
Katika Kipindi Chote Tangu Nchi Ilipopata Uhuru.
Mbowe Ameyasema Hayo Jana Wakati Akizungumza Na
Wahariri Wa Vyombo Vya Habari Kuhusu Hali Ya Kisiasa Kwa Mwaka 2017, Ambapo
Alisema Kila Mtu Ana Mapungufu Katika Utendaji Wake Wa Kazi Hivyo Kila Mmoja
Awe Tayari Kupokea Ushauri Kutoka Kwa Viongozi Wa Dini.
“Lakini Viongozi Wetu Wa Dini Wana Haki Ya
Kusema, Wana Wajibu Wa Kusema, Hawa Ni Watu Wanaolea Taifa Hili Kiroho, Huwezi
Kumshambulia Kakobe Kama Unamshambulia Mtoto Mdogo, Hawa Wana Waumini Wana
Followers (Wafuasi) Na Hawa Ndiyo Kila Siku Rais Anasema Wamwombee, Sasa
Wanamwombea Vipi Wakati Unawapa Masharti?,” Alisema Mbowe Na Kuongeza.
“Sisi Wapinzani Tunakosolewa, Viongozi Tuwe Na
Unyenyekevu Wa Kukubali Mawazo Tofauti Tukisemwa, Tusijenge Chuki Katika Jamii,
Vyama Vyetu Vyote Vinaongozwa Na Binadamu Vinaweza Vikakosea, Tuwaache Viongozi
Wa Dini Wafanye Kazi Yao, Tukikosea Waseme.”



