Mzee Majuto: Nilitabiri Magufuli Akiwa Rais Itakuwa Shughuli..Sasa Hivi Watu Wote Wana Adabu Zao

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli amemtembelea muigizaji mkongwe, Mzee Majuto
katika hospitali ya Tumaini jijini Dar es salaam ambako amelazwa akitibiwa.
Akizungumza mara baada ya kutembelewa
na Rais, Mzee Majuto amefunguka na kudai yeye ndio mtu wa kwanza kutabiri ujio
wa Rais Magufuli katika kuongoza nchi ya Tanzania huku akisisitiza kwamba
anajisikia faraja kuona ana misimamo iliyokuwa imara.

“Mimi ndiyo mtu wa kwanza kumtabiri kwamba akiwa Rais itakuwa shughuli.
Nilishukuru sana kuchaguliwa huyu bwana, tumepata Rais sio masihara watu wote
sasa hivi wana adabu zao wanajua nini maana ya kazi”,alisema Majuto.

Pamoja na hayo, Mzee Majuto aliendelea
kwa kusema ;“sisi
wazee tunafarijika sasa hivi, viwanda kila kona vimetapakaa na leo amekuja
kutembea hospitalini hapa sijui kama wengine hawajajikojolea huko kwa uoga
maana hataki masihara. Hii ndio raha ya kupata viongozi wenye msimamo”.

Kwa upande mwingine, Mzee Majuto
amesema sio rahisi kupata Rais mwenye misimamo na asiyekuwa na masihara kama
Dkt. John Magufuli.




