Video: Mbinu Mpya Inayotumika Kufanya Biashara Ya Ngono
Maambukizi ya Virusi vya Ukimwi
yameendelea kushika kasi kutokana na tabia mbalimbali hatarishi huku makundi
maalumu yakiwemo ya watu wanajidunga dawa za kulevya,watu kujihusisha na
mapenzi ya jinsia moja pamoja na biashara ya ngono 'ukahaba'.
Malunde1 blog imekutana na
Barthoromeo Zacharia jijini Mwanza, ambaye ni Mdau na Mshauri wa masuala ya
kiafya katika kupunguza madhara ya kiafya kwa jamii yanayotokana na VVU/ HIV,TB
na dawa za kulevya ambapo ameelezea namna biashara ya ngono hivi sasa inavyofanyika
kwa njia za kisasa na kusababisha maambukizi ya VVU kuendelea kuwepo.
Anasema pamoja na njia ya
wafanyabiashara ya ngono kujipanga katika barabara ama kupatikana katika maeneo
maalum/maarufu ya kufanyia biashara hiyo,pia kuna njia nyingine inayotumiwa na
wafanyabiashara hao,matokeo yake wanaume wanajikuta wanafanya ngono bila kujua
kuwa wanaofanya nao ni mahahaba.
"Huwezi kumtambua kwa urahisi mtu anayefanya biashara ya ngono kama hujakutana nae kwenye maeneo wanakofanyia,hivi sasa wanatumia mbinu ya 'Nauli', hukaa kwenye barabara,baa na maeneo mengine kisha hujirahisha kwa wanaume,wapo tayari kukufuata popote pale ulipo ukishashiriki nae ngono anakuomba pesa ya nauli,huo ndiyo ujira wake"- Source malunde 1
Msikilize Hapa
Akizungumza.



