Breaking News

Breaking News:Mzee Kingunge Ngombale Mwiru Afariki Dunia

Habari tulizozipokea hivi punde zinasema kuwa mwanasiasa mkongwe nchini Tanzania Mzee Kingunge Ngombale Mwiru amefariki dunia leo alfajiri Ijumaa Februari 2,2018 wakati akipatiwa matibabu katika hospitali ya taifa ya Muhimbili jijini Dar es salaam.

Mmoja wa wanafamilia ya Kingunge,Idd Janguo ameiambia Harakati Za Jiji kuwa mzee Kingunge amefariki dunia leo majira ya saa 10 alfajiri akieleza kuwa hali ya mzee ilibadilika tangu juzi.

Mzee Kingunge alikuwa kiongozi mwandamizi nchini Tanzania katika serikali za awamu nne zilizopita naamewahi kushika nyadhifa mbalimbali katika serikali  zikiwemo ukuu wa mikoa ya Tanga na Singida, Katibu Mwenezi wa Chama Cha Mapinduzi na Waziri katika wizara mbalimbali.

Ndugu Kingunge Ngombale Mwiru atakumbukwa kwa kulitumikia taifa la Tanzania kwa uadilifu mkuu na uzalendo uliotukuka unaofaa kuigwa na vizazi vya sasa na vijavyo. 

Taarifa zaidi zitafatia hivi punde...