Chadema Walimwa Barua... Kufanya Kampeni Nyumba Kwa Nyumba Kinondoni

Wakati
kampeni za uchaguzi jimbo la Kinondoni zikiendelea, Chadema wamepewa barua
mbili za malalamiko na msimamizi wa uchaguzi Wilaya ya Kinondoni, Aron
Kagurumjuli kikidaiwa kuvunja kanuni za maadili ya uchaguzi.
Akizungumza
Februari 1, 2018 Mkurugenzi wa Operesheni na Mafunzo wa Chadema, Benson Kigaila
amesema wamepokea barua hiyo jana, yenye malalamiko yaliyotolewa na Chama cha
Wananchi (CUF).
Katika
barua hiyo, CUF inalalamika kuwa Januari 28, Chadema walifanya kampeni nyumba
kwa nyumba katika eneo la Kigogo Mbuyuni hadi London Bar badala ya siku hiyo
kuwa kata ya Ndugumbi kama ratiba inavyoonyesha.
Malalamiko
mengine ni Chadema kudaiwa kutumia salama ya CUF katika majukwaa ya kampeni
sambamba na kupamba bendera za chama hicho.
"Madai
mengine ni kwamba viongozi wa CUF wanakuja katika mikutano yetu na kukaa meza
kuu na kupanda katika majukwaa. Pia CUF wanadai Chadema inawatumia viongozi wao
kupita nyumba kwa nyumba kuiombea kura Chadema wakiwa na sare za CUF,” amesema
Kigaila.
Kwa
mujibu wa barua hizo Chadema wanatakiwa kutoa maelezo ya utetezi kwa maandishi
kuhusu tuhuma hizo ndani ya saa 48 baada ya kuzipokea.



