JPM Ateua Mwanasheria Mkuu Wa Serikali Na Naibu Wake

Rais Magufuli amefanya uteuzi mpya
kwa kumteua Dk Adelardus Kilangi kuwa Mwanasheria Mkuu wa Serikali na Paul
Ngwembe kuwa Naibu Mwanasheria Mkuu wa Serikali.
Taarifa iliyotolewa na Katibu Mkuu
Kiongozi, Balozi John Kijazi, imeeleza kuwa Rais Magufuli pia amewateua
aliyekuwa Mwanasheria Mkuu wa Serikali George Masaju na Naibu wake, Gerson
Mdemu kuwa Majaji wa Mahakama Kuu, kuanzia Februari 1,2018.
Kabla ya uteuzi, Dk Kilangi alikuwa
Mkurugenzi wa Chuo Kikuu cha Mtakatifu Agustino (St. Augustine University)
kituo cha Arusha, na pia ni Mwenyekiti wa Bodi ya Mamlaka ya Udhibiti wa
Shughuli za Mkondo wa Juu wa Mafuta, (Tanzania Petroleum Upstream Regulatory
Authority- PURA).



