Breaking News

Sekta Binafsi Na Mchango Wa Kukuza Uchumi Wa Viwanda Nchini

Na Sala Mlawas
Shirika La Umoja Wa Mataifa La Maendeleo Ya Viwanda nchini ( UNIDO), limezindua nishati mbadala ambayo kusaidia wananchi kuondokana na swala la ukataji wa miti kwa ajili ya matumizi ya kuni.

Kauli hiyo imetolewa jijini Dar es salaam na Mratibu wa Shirika hilo Nchini Bw. Vikta Hakimu wakati akizungumza na waandishi wa habari ambapo amesema kuwa jumla ya kaya laki tano zinatarajiwa kunufaika na mradi huo.
Alisema kuanzishwa kwa mradi huo kutokana na serikali kuona kuendelea kuwepo na changamoto ya ukataji wa miti katika taifa hali ambayo itapelekea nchi kuwa jangwa.

‘kupitia mradi huo wameshirikiana na ofisi ya makamu wa raisi idara ya mazingira pia na wadau kutoka nje wa shirika la GF ( global environment facilities ) kwani mradi huo utapunguza adhari nyingi zinazoweza kujitokeza katika nchi na dunia kwa ujumla” Alisema Bw hakimu.

Kwa upande wake mkurugenzi wa bodi ya taasisi ya sekta binafsi, Bi Anna Matinde alisema wanaunga mkono mradi huo kwani itasaidia kuondoa changamoto mbalimbali zinazowakabili wanawake hususani katika swala la matumizi ya nishati ya kuni.


Bi Matinde aliongeza kuwa kupitia mradi huo ambao utatoa fursa na nafasi kubwa ya kuhamasisha wanawake wenzao faidi ya ya matumizi ya majiko hayo katika kipindi cha miaka minne cha utekelezwaji wa mradi huo Nchini.