Breaking News

Prof Mbalawa Azindua Shirika La Mawasiliano Tanzania, Asisitiza Ubunifu Na Wajibikaji

Image result for waziri mbarawa akizindua ttcl
Waziri wa  ujenzi uchukuzi na mawasiliano Prof. Makame Mbarawa amezindua sheria ya shirika la mawasiliano Tanzania.

Akiongeakatika hafla ya uzinduzi mapema leo jijini dar es salaam Prof. Mbarawa alisema kuwa uwepo wa sheria ya shirika la mawasiliano unatoa fursa ya kuboresha sekta kwa kuweka usimamizi wa miundombinu ya kimkakati nchini ukiwa chini ya shirika.

Aidha aliongeza kuwa shirka la umma la mawasiliano nchini ni muhimu kwa kwa ajili ya kulinda usalama wa nchi, kukuza uchumi na kutoa huduma za mawasiliano kwa jamii na katika ubora unaotakiwa.

Pamoja na hayo, Mbarawa aliongeza kuwa  kuanzia jana TTCL imebadilishwa kutoka kampuni kuwa shirika ili liweze kufanya kazi yake kwa weledi kwa maana utoaji huduma mbali mbali ambazo zimekuwa zikitolewa na TTCL jambo ambalo halitawaathiri wadau na watumiaji.

Mbarawa aliwatoa wasiwasi wafanyakazi wa iliyokuwa kampuni ya simu Tanzania kuwa wao pia watahamia katika shirika la mawasiliano kwa taratibu za kiutumishi kwa kuzingatia kifungu cha 29 cha sheria ya shirika.

Kutokana na mabadiliko hayo,shirika pia litaendelea kuwalipa mishahara na madai ya mishahara kwa waliokuwa wafanyakazi wa kampuni kulingana kifungu cha 30 cha sheria ya shirika sambamba na kuendelea na masuala ya michango ya mifuko ya hifadhi za jamii kama ilivyokuwa katika kampuni ya TTCL hapo awali.

''Nyaraka na kumbukumbu zote za kampuni ya TTCL zitahamishiwa kwenye shirika kwa mujibu wa sheria kifungu cha 31,'' alisema Mbarawa.

Hata hivyo Mbarawa alitoa rai kwa Taasisi za umma na binafsi ambao bado wanadaiwa na iliyokuwa kampuni ya TTCL kulipa madeni yao haraka iwezekanavyo na ameliagiza shirika hilo kukusanya madeni yote.

Mpaka sasa iliyokuwa kampuni ya TTCL inadaiwa zaidi ya bilioni mbili kutoka kwa taasisi za umma na binafsi.