ZARI Atangaza Rasmi Kumpiga Chini DIAMOND

Baada ya headlines za muda mrefu na mfululizo wa tetesi za penzi
la Zari na muimbaji wa
Bongofleva Diamond Platnumz kudaiwa
kuyumba, hatimae leo Zari ameamua
kuwatangazia mashabiki wake kuwa ameamua kuachana na Diamond Platnumz kwa madai ya
mfululizo wa matukio ya usaliti wa kimapenzi.
Zari ametangaza kuachana na Diamond Platnumz kupitia ukurasa
wake wa instagram na ameandika ujumbe mrefu ulioeleza sababu zote zilizomfanya
kufikia maamuzi hayo licha ya kuwa yeye na Diamond wamezaa watoto wawili Nillan na Tiffah,
kupitia ukurasa wake wa instagram Zari ameandika
hivi.
![]() |
“Elewa kuwa hiki ni kitu kigumu sana kwangu kukifanya, kumekuwa na
tetesi mbalimbali baadhi kati ya hizo zimekuwa na ushaidi ambao umekuwa
ukisambaa katika vyombo vya habari kuhusiana na usaliti wa kimapenzi unaofanywa
na Diamond, kwa huzuni nimeamua kuvunja uhusiano wangu wa kimapenzi na Diamond
kwa heshima yangu”
“Tunaachana
kama wapenzi lakini sio kama wazazi hii hainipunguzii mimi kuwa mtu wa
kujitegemea, mama mwenye kujali na Boss Lady, wote mnatakiwa kufahamu hilo
nitaendelea kujijenga kama mwanamke mwenye ushawishi, nitawaamasisha wanawake
wote kuwa maboss Ladies”
“Nitawafundisha watoto wangu wanne wa
kiume kuwaheshimu wanawake na nitamfundisha binti yangu ni nini maana ya
heshima, nimekuwa katika kiwanda cha burudani kwa miaka 12 sasa pamoja na
changamoto zote hizo lakini nimefanikiwa kuwa mshindi kwa sababu mimi ni
mshindi nawatakiwa wote siku njema ya wapendanao”
Kama utakuwa unakumbuka vizuri Zari na Diamond walianza
kudaiwa kuwa hawapo pouwa katika mahusiano yao toka kuvuja kwa clip video
iliyokuwa inadaiwa kuwa Diamond alimpeleka
msichana mwingine kulala nae Madale lakini
tukio la Diamond kunaswa
na camera za mapaparazi akikumbatina na mpenzi wake wa zamani Wema Sepetu wakati wa utambulisho
wa Mbosso kama
msanii mpya wa WCB, kitendo
kile kilidaiwa kuwa hakikumpendeza Zari.
![]() |





