Morgan Tsvangirai Afariki Dunia

Na mashirika ya kimataifa
KIONGOZI mkuu wa upinzani nchini Zimbabwe, Morgan Tsvangirai
amefariki dunia usiku wa jana.
Amefariki katika hospitali moja nchini Afrika Kusini
alikokuwa akipatiwa matibabu ya saratani ya utumbo.
Naibu Mwenyekiti wa chama cha MDC, Elias
Mudzuri kupitia ukurasa wa twita alitangaza kifo hicho.
"Ninauzuni kutangaza kumpoteza mpambanaji
na mpigania demekrasia," ameandika
Tangu mwaka 2016 Tsvangirai alikuwa akienda
Afrika Kusini kupatiwa matibabu ya kansa.



