DIAMOND: Media Zinazokataa Kupiga Nyimbo Zangu Zinapotea

Mwanamuziki wa
Bongo fleva na CEO wa label ya WCB, Diamond Platnumz amefunguka na kusema kuwa
chombo chochote cha habari ambacho kinaibania WCB kwa njia yoyote basi
kitapotea kwani yeye ni kama maji usipokunywa utayaoga.
Diamond amekuwa
mmoja wa wasanii ambaye amekuwa na migogoro na media mbali mbali ambapo siku za
hivi karibuni Kumekuwa na sintofahamu kati yake na mkurugenzi wa Clouds Fm,
Ruge Mutahaba.
Hii imekuja baada
ya Diamond kutangaza kuanzisha stesheni zake za redio na Tv ambazo ni Wasafi
Radio na Tv ambavyo amesisitiza vitacheza nafasi kubwa katika kukuza mziki wake
na hata wasanii kutoka WCB kwa ujumla.
Diamond hivi sasa
yuko nchini Kenya, Nairobi ambako ameenda kwenye uzinduzi wa albamu yake ya ‘A
boy from Tandale’ ambayo inategemewa kuanza kuuzwa hivi karibuni.
Kwenye mahojiano
na Dizzim Online, Diamond amefunguka kuhusu albamu yake ambayo ndani yake kuna
nyimbo ambazo amewashirikisha wasanii kadhaa ikiwemo Rick Ross, Neyo na
Omarion.
Lakini pia Diamond
amefunguka kuhusu Wasafi Tv na Redio ambavyo vinategemea kuanza kuruka hewani
siku za hivi karibuni lakini Diamond ameshangaa media zinazotaka kubania mziki
wake kwani yeye ndio burudani yenyewe kwaiyo wao kumzuia yeye wanapotea:
"Yaani mimi
nimejiwekea mazingira ambayo hata nikilala chumbani lazima utaniongelea huwezi
kulala bila kunitaja aidha utawataja watoto wangu, au wasanii wa WCB au hata
wapenzi wangu yaani Diamond ni kama Azam vile au mimi kama maji aidha utaninywa
au utanioga yaani utajua mwenyewe lakini mimi huwezi kulala bila kunitaja
kwaiyo media zinazozuia kazi zangu wanapoteza muda maana mimi ndio burudani na
mzalisha burudani”



