Breaking News

LIPUMBA: CUF Tumemdekeza Sana Maalim Seif

Mwenyekiti wa CUF anayetambuliwa na Ofisi ya Msajili wa Vyama vya Siasa, Profesa Ibrahim Lipumba amesema chama hicho kilimdekeza kwa kiasi kikubwa Katibu mkuu wake, Seif Sharif Hamad.
Profesa Lipumba ametoa kauli hiyo leo Jumapili Machi 18, 2018 wakati akifungua kikao cha kwanza cha kawaida cha Baraza Kuu la Uongozi la CUF kinachofanyika makao makuu ya chama hicho, Buguruni jijini Dar es Salaam.
Alisema mambo na hatua ambazo amekuwa akizichukua Maalimu Seif zimepelekea CUF kushindwa kupata viongozi watakaoingia katika Baraza la Wawakilishi la Zanzibar sambamba na kutokuwepo kwenye Serikali ya Umoja wa Kitaifa (SUK).
“CUF tumemdekeza kwa muda mrefu na zile nyimbo tulizokuwa tukiimba ya kuwa akipata Seif tumepata sote zilikuwa zimemuingia kichwani kwelikweli na yeye alitafsiri kuwa akikosa Seif tumekosa sote,” Alisema Profesa Lipumba.
Alisema Matokea yake tumekosa kuwa na uwakilishi katika Baraza la Uwakilishi jambo ambalo limetuathiri kisiasa hasa Zanzibar. Hili kosa kubwa tuliowakosea Wazanzibari”
Aidha  Profesa lipumba pia alieleze ziara yake ya Pemba imesaidia kuimarisha chama hicho na hivi sasa wananachi na viongozi wa CUF wanaijua vyema Katiba ya chama tofauti na hapo awali.