Breaking News

Manispaa Ya Temeke Yapongezwa Kukarabati Kituo Cha Mabasi Ya Mikoani Mbaraga Rangi Tatu

Na Sala Mlawas
Halimashauri ya manispaa ya Temeke jijini dar es salaam imepongezwa kwa kutoa mkataba katika kituo cha mabasi ya mikoani kilichopo mbagala rangi tatu.

Akizungumza na waandishi Wa habari Jijini Dar Es Salaam Mjumbe Wa Mabasi Ya Mikoani Bw Hamisi Hemed Alisema mkataba huo watasaidia kutatua kero mbali mbali zilizokuwa zinawakabili wasafiri wanaotumia kituo hicho.

Alisema kupitia mkataba huo tayali wameanza kuchukua hatua mabalimbali ikiwemo kumwaga vifusi katika kituo hicho kwa lengo la kuboresha kituo hiko kwa kushirikiana na manispaa ambayo tayali imetoa nyenzo (Vifaa) vya kusambaza vifusi hivyo.

“Tutakutana kupanga namna ya kutatuoa changamoto zinazokikabili kituo hicho ikiwezekana washirikiane na taasisi za kifedha kama mabenki waweze kutukopesha ili barabara zilizopo katika kituo hicho zitengenezwe kiwango cha zege au cha kokoto” Alisema Bw. Hemed .

Aidha Wafanyabiashara wanaofanya biashara zao katika kituo hicho wakiongea na mwandishi wa mtandao huu Bi. Nuru Mshamo na Bi Time ameipongeza halimashauri kwa kuweza kuungana na uongozi wa kituo hicho (UMAKUTA) kwa jitihada wanazofanya kuboresha kituo hicho kutokana na kituo hicho kuwa moja ya chanzo cha kujipatia kipato kinachosaidia kujikimu  wao na familia zao.

“Katika kipindi kirefu kituo hichokimekuwa na kinakabiliwa na changamoto kubwa zilizokuwa zikiwakabili wafanyabiashara hao hususani kuhamishwa kwa mabasi madogo katika kituo hiko kwani wao wateja wao wakubwa ni madereva na makondakta kwa ununuzi wa vyakula vyao” Aliesma Bi Nuru.

Walisema  kufatia kuboreshwa  kwa miundombinu  ya kituo hicho hususani Barabara zitasaidia kuwa chachu kwa ongezeko la wateja kwani eneo likiwa zuri watu wanakuja kwa wingi.