Maonyesho Ya Young Scientists Tanzania (YST) 2018 Kufanyika Mwezi Agosti
Mwanzilishi Mwenza wa Young Scientists Tanzania (YST) Dk.Gosbert Kamugisha (kulia). akizungumza katika mkutano na waandishi wa habari kuhusu maonyesho ya Young Scientists Tanzania (YST) 2018 yatakayofanyika mwezi Agosti mwaka huu Ukumbumbi wa Mwalimu Nyerere International Convention center (JNICC) jijini Dar es salaam, Wengine kutoka kushoto Bi. Patricia Mhondo kutoka kampuni ya Shell Explorstion and Production Tanzania LTD (Shell) na Joseph Clawry Kutoka ubalozi wa Irand nchini.
Meza Kuu pamoja na
wadhamini wa maonyesho hayo.
Mkurugenzi
wa Karimjee Jinanjee Foundation (KJF), Yusuf Karimjee akizungumzia
udhamini wao
Patricia Mhondo kutoka
Kampuni ya Shell Explorstion anda Production Tanzania ltd (Shell) akizungumza kwenye mkutano huo.
Joseph Clawry kutoka
nchi ya Iland akizungumzia kazi za ubunifu na jinsi nchi yao inavyowawezesha
wanafunzi waliofanya vizuri katika miradi yao.
Na
Dotto Mwaibale
MAONYESHO
ya Young Scientists Tanzania (YST) 2018 yatafanyika mwezi Agosti mwaka huu
Ukumbi wa Julius Nyerere International Convention Centre (JNICC) jijini Dar se
Salaam.
Akizungumza
na waandishi wa habari Dar es Salaam jana Mwanzilishi Mwenza wa YST, Dk.
Gosbert Kamugisha alisema maonesho hayo yatafanyika kuanzia tarehe moja hadi
mbili mwezi huo.
"Wanafunzi
wote wanaopenda kushiriki wanashauriwa kutuma kazi za miradi yao kwenda YST
kabla ya tarehe 21 Aprili 2018" alisema Kamugisha.
Kamugisha
alisema wanafunzi 200 watakaochaguliwa wataonyesha kazi za teknolojia na
ugunduzi wa kisayansi kwenye onesho hilo la mwaka huu na kuwa na wanafunzi
watakaochaguliwa watapewa mafunzo kutoka kwa washauri wa sayansi wa YST kuhusu
namna ya kutengeneza kazi zao za kisayansi.
Alisema
onesho hilo pamoja na mpango wa kuzitembelea shule na wanafunzi kuwapatia
ushauri wa kisayansi vinawezeshwa na wadhamini wakuu wa YST ambao ni Shell
Explorstion snd Production Tanzania Ltd (shell) na Karimjee Jinanjee Foundation
(KJF)
"Tunapenda
kuwashukuru wadhamini wetu tangu mwaka 2012. Mwaka huu wa 2018 KJF wameongeza
kiwango cha udhamini na kuwa mmoja wapo wa wadhamini wakuu wa YST kwa kipindi
cha miaka mitano ijayo.
Alisema
udhamini huo utaiwezesha programu ya YST kuwa endelevu na kuwawezesha vijana
kufanya ubunifu na kufanya tafiti za kisayansi ili kuleta maendeleo ya kijamii
na kiuchumi.
Kamugusha
aliongeza kuwa wanasayansi chipukizi wakaoshiriki onesho la YST mwaka huu kwa
sasa wanaendelea kutengeneza kazi za miradi yao katika nyanja mbalimbali za
kisayansi kama kemia, fizikia na hesabu, biolojia na ekolojia, saynsi ya jamii
na teknolojia na kuwa kazi miradi nyingi zimejikita katika sekta ya afya,kilimo
na usalama wa chakula, mawasiliano na usafirishaji, nishati,elimu, mazingira na
mabadiliko ya tabia nchi.
Alisema
wanafunzi watakajituma na kufanya ugunduzi mzuri watazawadiwa pesa taslimu,
medali, vikombe na uimarishaji wa maktaba ya shule yao kama ambavyo wamefanya
kwa miaka sita iliyopita KJF watawazadia wanafunzi wenye ugunduzi mzuri zaidi
zawadi za udhamini wa masomo ya chuo kikuu ili kuwawezesha kusoma masomo ya
sayansi na teknolojia katika ngazi ya chuo kikuu.



