Sababu 6 za Kukamatwa Mchungaji KKKT
SABABU sita zinadaiwa kuwa ndio chanzo
cha mchungaji Fredy Njama wa Usharika wa Karanga, KKKT Dayosisi ya Kaskazini,
Moshi aliyekamatwa na Polisi kwa kinachodaiwa kuwa ni “Uchochezi”.
Mchungaji huyo
wiki mbili zilizopita alisoma ripoti katika mkutano mkuu wa mwaka wa usharika
wake ambayo ndo imepelekea kukamatwa kwake.
Katika ripoti
hiyo, alibainisha kuwa mapato ya usharika yanapungua kwa sababu mbalimbali.
Katika utangulizi wa ripoti hiyo alitaja changamoto sita zinazoikabili nchi kwa
sasa:
- Ukosefu wa ajira
kwa vijana
- Hali ya uchumi inayoyumba
- Hali ya kisiasa ni ya mashaka
- Gharama kubwa za matibabu
- Sera ya elimu bure
- Wastaafu kutolipwa mafao yao.
- Hali ya uchumi inayoyumba
- Hali ya kisiasa ni ya mashaka
- Gharama kubwa za matibabu
- Sera ya elimu bure
- Wastaafu kutolipwa mafao yao.
Ripoti hiyo pia
imechapwa ktk kijitabu na kiwanda cha uchapaji cha Dayosisi hiyo.
Kundi la Polisi na
maafisa usalama walimchukua Ijumaa asubuhi hadi kiwandani na kumtaka akusanye
vijitabu vyote hadi vilivyosambazwa na kuvikabidhi Polisi. Aidha walimtaka
aandike barua kuomba radhi na kufuta ripoti hiyo.
Jioni ya juzi, Polisi walifika ofisi ya usharika na kufanya upekuzi. Walichukua laptop na flash. Kisha walimpakia mchungaji katika gari lao na kuondoka naye.




