Naibu Spika Tulia: Sina Hakika Kama Mange Kimambi Ni Binadamu Wa Kawaida

Naibu Spika wa
Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Tulia Ackson amefunguka na
kusema kuwa yeye hana uhakika kama mwanadada mwanaharakati wa mitandaoni Mange
Kimambi kama ni binadamu wa kawaida kama yeye.
Tulia Ackson
amesema hayo alipohojiwa na moja ya chombo cha habari na kusema kuwa kwa sasa
hawezi kusema kama mwanadada huyo anakosea au laa kwa kuwa hana uhakika kama
yupo kama yeye na kusema labda akipata fursa ya kuonana naye na kuona kweli
yupo kama yeye ndiye anaweza kuwa na la kusema.
"Sina hakika
kama yeye ni binadamu wa kawaida kama mimi kwa hiyo sijui labda nikikutana naye
ndiyo nitajua chakuzungumza naye lakini kwa yale nayoyasikia hapa na pale sina
hakika kama yeye ni binadamu wa kawaida kama mimi ila kama yupo kama mimi basi
nitapata fursa ya kumshauri nikionana naye.
"Siwezi
kusema anakosea kama nilivyosema sijajua yeye ni mtu wa namna gani kwa hiyo
huenda hakosei labda ni aina yake ya binadamu yaani ni specie tofauti hivyo
kama yeye ni specie ya tofauti huwezi kusema anakosea" alisema Tulia
Ackson
==>Msikilize Hapo



