Maabara Ya Kisasa Ya TFDA Kanda Ya Ziwa Kuleta Ahueni Kwa Wananchi
Wafanyabiashara
wakiwemo wazalishaji wa bidhaa mbalimbali Kanda ya Ziwa, wametakiwa kuitumia
vyema Maabara ya Kisasa ya Mamlaka ya Chakula na Dawa TFDA iliyopo Jijiji
Mwanza ili kufanya uchunguzi wa bidhaa zao kabla ya kuziingiza sokoni.
Katibu Mkuu Wizara ya Afya, Maendeleo
ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt.Mpoki Ulisubisya akizungumza mara baada ya ziara ya kukagua ufungwaji wa mashine za maabara hiyo,
kujionea utendaji pamoja na kuzungumza na wafanyakazi wa TFDA.
Kaimu Mkurugenzi Mkuu TFDA, Bi. Agnes
Kijo alisema uwepo wa maabadara ya hiyo Kanda ya Ziwa, utasaidia uchunguzi wa
bidhaa mbalimbali kukamilika kwa wakati na hivyo kuwaondolea usumbufu
wazalishaji wa bidhaa hizo wakiwemo wenye viwanda vidogo vidogo.
Serikali kwa kushirikiana na taasisi
ya Global Fund imefanikisha upatikanaji wa mashine za kisasa katika ofisi za
TFDA Kanda ya Ziwa pamoja na Makao Makuu vilivyogharimu zaidi ya shilingi
bilioni tano.



