Waziri Ummy Azindua Dawa Ya Kutibu Kifua Kikuu Kwa Watoto Wadogo Jijini Dar
Waziri wa Afya,Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Ummy
Mwalimu akiongea na baadhi ya wadau wa Sekta ya afya (hawapo pichani) wakati wa
uzinduzi wa dawa ya kutibu kifua kikuu kwa watoto wadogo kueleka maadhimisho ya
siku ya Kifua Kikuu tarehe 24 Machi 2019.
Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Ummy
Mwalimu kushoto akimuangalia mtoto Salome katikati akinywa dawa ya Kifua Kikuu
wakati wa uzinduzi wa dawa ya kutibu kifua Kikuu kwa watoto wadogo leo jijini
Dar es salaam, kutoka kulia ni Mratibu wa Kupambana na Magonjwa ya Kifua Kikuu
na Ukoma Dkt. Beatrice Mutayoba, anayefuata aliyevaa kitenge ni mzazi wa
Salome Bi. Upendo Jeremiah.
Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Ummy
Mwalimu kushoto akionyesha dawa kutibu Kifua Kikuu kwa watoto wadogo wakati wa
uzinduzi wa dawa hiyo leo jijini Dar es salaam kueleka maadhimisho ya siku ya
Kifua Kikuu tarehe 24 Machi 2019.
Mganga Mkuu wa Serikali Prof. Mohammed Bakari Kambi baadhi ya wadau wa
Sekta ya afya hawapo pichani wakati wa uzinduzi wa dawa ya kutibu kifua kikuu
kwa watoto wadogo kueleka maadhimisho ya siku ya Kifua Kikuu tarehe 24 Machi
2019 iliyofanyika leo jijini Dar es salaam.
Baadhi
ya wadau wa Sekta ya afya wakifuatilia kwa makini Waziri wa Afya,Maendeleo ya
Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Ummy Mwalimu (hayupo pichani) wakati wa
uzinduzi wa dawa ya kutibu kifua kikuu kwa watoto wadogo kueleka maadhimisho ya
siku ya Kifua Kikuu tarehe 24 Machi 2019 .
NA
WAMJW-DAR ES SALAAM.
SERIKALI kupitia Wizara ya Afya imetenga shilingi bilioni 5 kwa ajili ya
kununua mashine za kupima vipimo vya ugonjwa wa kifua kikuu katika zahanati na
vituo vya afya nchini.
Hayo yamezungumzwa na Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee
na Watoto Mhe. Ummy Mwalimu wakati wa uzinduzi wa dawa za kutibu ugonjwa wa
Kifua Kikuu kwa watoto kuanzia umri wa miaka 14 kushuka chini leo jijini Dar es
salaam.
“Serikali imadhamiria kupambana na ugonjwa wa Kifua Kikuu hivyo tumetenga
shilingi bilioni 5 kwa ajili ya kuongeza mashine nyingine za kufanya uchunguzi
kwa haraka vya ugonjwa wa Kifua Kikuu zinazoitwa Genexpert ” alisema
Waziri Ummy.
Aidha Waziri Ummy amesema kuwa marufuku kwa watoa huduma kutoa matibabu
ya Kifua Kikuu kwa gharama yoyote kwani huduma hiyo ni bure.
Kwa mujibu wa Waziri Ummy amesema kuwa marufuku kwa waganga wa kienyeji
kuwashikilia wagonjwa wa Kifua kikuu na badala yake wawaruhusu waende hospitali
kwa ajili ya msaada wa haraka.
Aidha, Waziri Ummy amesema kuwa takribani watu laki moja na 60 wana
maambukizi ya ugonjwa wa kifua kikuu kwa makadirio ya mwaka 2016.
Sambamba na uzinduzi wa dawa hizo Waziri Ummy amegawa mashine nyingne za
Genexpert kwa ajili ya kufanyia uchunguzi wa makohozi ili kugundua kuna
maambukizi au hapana kwa hospitali za ,Kairuki, Agakhan, Regency ,
TMJ na Indumandal ambazo kila mashine moja inagharimu shilingi milioni 34 .
Aidha Waziri Ummy ametoa rai kwa wazazi na walezi wa watoto kwenda
hospitali mara wanapoona dalili moja wapo ya TB ikiwemo kuumwa mara kwa mara
kwa muda wa wiki mbili, kukosa furaha, mtoto kulia mara kwa mara, kupungua
uzito , kuchelewa kukua na kikohozi cha mara kwa mara.








