Halmashauri Ya Temeke Kinara Vitendo Vya Rushwa
Mkuu wa Takukuru mkoa wa Temeke Pilly Mwakasege, akizungumza na
waandishi wa habri (Hawapo Pichani) jijini Dar es Salaam.
Na Mwandishi wetu.
TAASISI ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa
(Takukuru) Mkoa wa Temeke, imesema Halmashauri ya Manispaa ya Temeke inaongoza
kulalamikiwa kwa kukidhili kwa vitendo vya rushwa katika kipindi cha mwezi Oktoba
2017 hadi Machi 2018.
Akizungumza
na waandishi wa jijini Dar es Salaam Mkuu wa Takukuru mkoani wa Temeke Bi. Pilly
Mwakasege alipokuwa akielezea utekelezaji ofisi inavyotekeleza majukumu yao juu
katika kipindi hicho.
“Kati
ya malalamiko 232 yaliyopokelewa na ofisi ya Takukuru Temeke kwa kipindi cha
Oktoba 2017 hadi Machi 2018, eneo linaloongoza kwa kulalamikiwa kwa vitendo vya
rushwa ni Halmashauri ya Manispaa ya Temeke, ambapo malalamiko 87 yalipokelewa
na kufanyiwa kazi,” alisema Mwakasege.
Mwakasege
alisema eneo linalofuatia kwa kulalamikiwa kwa vitendo hivyo ni sekta binafsi
ambapo ofisi imepokea malalamiko 52 ikifuatiwa na Mahakama 37, polisi 26 na
Idara nyingine malalamiko yalipokelewa na yanaendelea kufanyiwa uchunguzi.
Alisema
kutokana na malalamiko hayo wameshafungua majalada ya uchunguzi 146 ambapo kati
ya hayo, majalada 18 yanaendelea na uchunguzi wa kina na 60 yanaendelea na
uchunguzi wa awali ili kubaini makosa ya rushwa na kuwafikisha watuhumiwa
mahakamani watakapothibitika.
Pia
Bi Mwakasege aliongeza kuwa majalada 68 yalifanyiwa uchunguzi wa awali na
kuthibitika kutokuwepo kwa viashiria vya rushwa hivyo yalifungwa.
Mkuu
huyo amesema taarifa 86 ambazo zilipokelewa na kuonekana kuwa zinatokana na
wananchi kutoelewa utaratibu wa kiutendaji katika Idara mbali mbali za
serikali, wananchi walishauriwa utaratibu wa kufuata na kutafutiwa ufumbuzi wa
malalamiko yao.
Aidha
amesema katika kipindi hicho pia kiasi cha sh. 44,478,901.59 kimeokolewa kutoka
sehemu tofauti, ikiwa sh. 15,794,489.59 ni mishahara hewa katika halmashauri ya
manispaa ya Temeke n ash. 1,000,000 ni marejesho ya malipo kutoka mfuko wa
jimbo la Temeke na sh. 27,684,412.02 ni marejesho ya malipo ambayo hayakufuata
utaratibu wa zabuni katika Chuo cha Taasisi ya Uhasibu Tanzania (TIA).
Ameleza
kuwa wameweza kufungua jumla ya kesi sita mpya mahakamani huku hadi kufukia
mwezi Machi 2018 jumla ya mashauri saba yaliendelea kusikilizwa mahakamani
yakiwa katika hatua mbalimbali ambapo kati ya hayo, Manispaa ya Temeke idara ya
afya ni moja.
Mengine
ni Idara ya Elimu Manispaa ya Temeke moja, TRA-Kigamboni moja, Manispaa ya
Ilala Idara ya Ustawi wa Jamii moja, Manispaa ya Kigamboni Idara ya Afya moja,
na watu binafsi shauri moja. Vile vile shauri moja limetolewa maamuzi
mahakamani ambapo Takukuru Temeke ilishinda.
Katika
kuhakikisha wanadhibiti mianya ya rushwa, Mwakasege amesema wanalojukumu la
kufuatilia matumizi ya fedha za miradi ya maendeleo, kufanya uchambuzi wa
mifumo (System Analysis) , kufanya vikao/warsha za kujadili mianya ya rushwa na
kuweka maazimio ya kuziba/kupunguza mianya hiyo pamoja na kufuatilia
utekelezaji wa maazimio hayo.
Ameongeza
pia wataendelea kutoa elimu ya rushwa kwa umma, lengo likiwa ni kuwapa wananchi
uelewa kuhusu rushwa, haki na wajibu wao katika kupambana na vitendo hivyo,
pamoja na kuelewa mahali na njia ya kuwasilisha malalamiko yao kuhusu vitendo
vya rushwa.



