Askofu MBEDULE Aomba Radhi

Askofu wa Kanisa la Kiinjili la
Kilutheri Tanzania (KKKT) Dayosisi ya Kusini Mashariki, Dk Lucas Mbedule
amewaomba radhi waumini wa dayosisi hiyo na Baraza la Maaskofu kwa kutokusoma
waraka uliotolewa wa sikukuu ya Pasaka.
Askofu Mbedule ameomba radhi leo
Aprili 29, 2018 wakati wa Ibada ya iliyofanyika kanisa la Mtwara Mjini, amesema
licha ya salamu hizo kutokusomwa, anaunga nazo na yupo pamoja na maaskofu
wenzake.
Akisoma barua ambayo ameituma kwa
Mkuu wa KKKT, Askofu Dk Fredrick Shoo na maaskofu wote wa kanisa hilo, Askofu
Mbedule amesema baraka za mababa maaskofu zilishindwa kusomwa kwa sababu
zilizojitokeza wakati huo.
“Kwa njia ya barua hii, kwanza
napenda kuwaombeni radhi kwa kuwakosesha baraka za mababa maaskofu,” amesema
Askofu Mbedule.
Amesema yeye alishiriki kuuandaa na
kutia saini na yupo pamoja na maaskofu wenzake.



