Mahakama Yatoa Amri Hans Pope Wa Simba Kukamatwa

Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu leo
Jumatatu imetoa amri ya Mwenyekiti wa Kamati ya Usajili ya Simba,
Zacharia Hans Poppe na Franklin Lauwo wakamatwe na wafikishwe mahakamani hapo
kuunganishwa katika kesi ya utakatishaji fedha inayomkabili rais wa timu
hiyo, Evans Aveva na makamu wake, Geofrey Nyange ‘Kaburu’.
Aveva na Kaburu wanakabiliwa na
mashtaka matano ya kughushi, kuwasilisha nyaraka ya uongo na kutakatisha
fedha kiasi cha dola 300,000 za Kimarekani.
Amri hiyo imetolewa na hakimu mkazi
mkuu wa mahakama hiyo, Thomas Simba baada ya wakili Taasisi ya Kuzuia na
Kupambana na Rushwa nchini (TAKUKURU), Leonard Swai kubadilisha hati ya
mashtaka na kuwaongeza watuhumiwa hao.
Swai alidai kuwa amewatafuta
washitakiwa hao toka machi tatu mwaka huu bila mafanikio na kuomba hati
ya kuwakamata washitakiwa hao ambao hawakuepo mahakamani.



