MAKAMU WA RAIS MHE. SAMIA SULUHU HASSAN AZINDUA CHANJO YA SARATANI YA MLANGO WA KIZAZI
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akifungua mkutano wa chanjo ya
kukinga Saratani ya Mlango wa Kizazi uliofanyika mapema leo katika viwanja vya
Mbagala Zakim jijini Dar es salaam.
Waziri
wa Afya , Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Ummy
Mwalimuakimkaribisha mgeni rasmi Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan wakati wa uzinduzi wa chanjo ya
kukinga Saratani ya Mlango wa Kizazi.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiangalia Chanjo ya kukinga
Saratani ya Mlango wa Kizazi baada ya kukabidhiwa na wataalamu wa masuala ya
Afya, wa kwanza kushoto ni Waziri wa Afya , Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee
na Watoto Mhe. Ummy (MB).
Makamu
wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan
akikata utepe ishara ya uzinduzi rasmi wa Chanjo ya kukinga Saratani ya Mlango
wa Kizazi shughuli iliofanyika mapema leo katika viwanja vya Mbagala Zakim
jijini Dar es salaam.
Makamu
wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan
akipokea sindano ya chanjo ya kukinga Saratani ya Mlango wa Kizazi kutoka mtoa
huduma za Afya, kulia ni Waziri wa Afya , Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na
Watoto Mhe. Ummy (MB).
Picha
ya pamoja ikiongozwa na Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Mhe. Samia Suluhu Hassan wakati wa uzinduzi wa chanjo ya kukinga
Saratani ya Mlango wa Kizazi uliofanyika mapema leo katika viwanja vya Mbagala
Zakim jijini Dar es salaam.
Picha
ya pamoja ikionesha baadhi ya wanafunzi wa shule za msingi waliohudhuria
kumuunga mkono Mhe. Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Mhe. Samia Suluhu Hassan wakati wa uzinduzi wa chanjo ya kukinga
Saratani ya Mlango wa Kizazi.
NA
WAMJW-Dar Es Salaam
MAKAMU
wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan
amezindua chanjo ya kukinga Saratani ya Mlango wa Kizazi ili kutokomeza vifo
vitokanavyo na magonjwa hayo nchini.
Katika
ufunguzi huo uliofanyika leo jijini Dar es salaam Makamu wa Rais Mhe. Samia
Suluhu Hassan amesema kuwa chanjo hiyo imewalenga wasichana wote wanaotimiza
umri wa miaka 14 ili kuanza kujikinga mapema na ugonjwa huo.
"Ili
kupata kinga kamili, wasichana watahitajika kupata dozi mbili ambapo dozi
ya kwanza itatolewa muda wowote binti anapofikisha umri wa miaka 14 na dozi ya
pili itatolewa miezi site baada ya kupata dozi ya kwanza" alisema Mhe.
Samiah Suluhu.
Aidha,Mhe.
Samia amesema kuwa chanjo hiyo ya kukinga saratani ya mlango wa kizazi
inatolewa bila ya malipo pamoja na uchunguzi wake kwani Serikali
imedhamiria kutokomeza tatizo hilo nchini.
"Niwaagize
Waganga wa Mikoa na Wilaya kuandaa kambi za wazi angalau mara tatu kwa mwaka
ili kutoa huduma hiyo tena bila ya malipo kwa wanawake na wasichana wote
nchini" alisisitiza Makamu wa Rais Mhe. Samia Suluhu.
Mbali
na hayo Mhe. Samia Suluhu amesema kuwa takribani wasichana laki 616, 734
wanatarajia upata chanjo ya kukinga saratani ya mlango wa kizazi kwa mwaka 2018
na chanjo hiyo imethibitishwa na Shirika la Afya Duniani(WHO).
Kwa
upande wake Waziri wa Afya , Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe.
Ummy Mwalimu amesema kuwa chanjo hii itakuwa ya saba kati ya chanjo ambazo
zinatolewa kwa watoto ili kuwakinga na magonjwa mbalimbali.
"Ukiacha
chanjo ya kukinga Saratani ya mlango wa Kizazi, hapa nchini chanjo nyingine
zinazotolewa ni ya kifua kikuu, Polio, Nimonia, Kuharisha ama Rota, Surua
na Rubella , Donda Koo, Kifaduro, Homa ya Ini, Uti wa mgongo na Pepopunda kwa
watu wazima" alisema Waziri Ummy.
Aidha,
Waziri Ummy amesema kuwa Serikali imefanikiwa kuweka maghala kuhifadhia
chanjo katika mikoa yote nchini ambayo yana uwezo wa kuhifadhi chanjo kwa miezi
sita bila ya kuharibika.
Kwa
Mujibu wa Waziri Ummy amesema kuwa zawadi za fedha taslimu zitatolewa kwa Mikoa
mitatu itakayofanya vizuri katika utoaji wa chanjo ya kukinga saratani ya
mlango wa kizazi hapa nchini.
Kwa
upande wake Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Mhe. Paul Makonda amesema kuwa
wananchi wajitokeze kwa wingi kwenye vituo vya kutolea huduma za afya ili
kwenda kupata vipimo na chanjo za kukinga saratani pindi wanapogundulika wana
magonjwa hayo.
"Natoa
rai kwa wananchi mliojitokeza hapa kuwapeleka watoto zenu wake zenu na wanawake
wote hususan wasichana wenye umri wa miaka 14 kwenda kupata chanjo hii na
mkifika majumbani kwenu muwakumbushe watu wenu wa karibu kushiriki katika
upataji wa chanjo hii" alisema Mhe. Makonda.



