WAKAZI KATA YA KEKO MWANGA B WASISITIZWA KUZINGATIA USAFI
Mwenyekiti Wa Kata Ya Keko Mwanga B, Bw. Shilingi Hashimu Shilingi
Na Sala Mlawas
Wananchi Wa Kata Ya Keko Manispaa Ya Temeke
Jijini Dar Es Salaam wameshauliwa kusafisha mazingira
hususani katika maeneo wanayoishi na maeneo yote yanayo wazunguka jambo ambalo
litasaidia kuondoa mazalia ya Mbu .
Akizungumza jijini Dar Es Salaam
Mwenyekiti Wa Kata Ya Keko Mwanga B, Bw. Shilingi Hashimu Shilingi alisema wakazi
wa kata hiyo wanatakiwa kuzingatia usafi wa mazingira hususani mifereji kwa
kufanya hivyo kutasaidia kundoa mazalia ya mbu sambamba na kutatua kero kubwa
ya mafuriko katika makazi ya wananchi.
“Kumekuwepo na taarifa kuwa katika kiwanda kilichopo
katika kata hiyo kuna wagonjwa wawili ambao inaelezwa kuwa wamedhibitika
kuwa na ugonjwa Wa dengue anawaasa wananchi wachukue tahadhari kwani
ugonjwa huo ambao dalili zake kama za maleria hivyo basi wananchi
wajitahidi kusafisha maeneo yote yanayowazunguka na kuondoa mazalia ya mmbu”
Alisema Bw. Hashimu.
Aidha Bw. hashimu aliongeza kuwa katika
kipindi hiki cha msimu cha mvua kumekuwepo na
magonjwa yanayojitokeza hususani magonjwa ya milipuko hivyo kuwataka
wananchi kufata kanuni za usafi kwa kuchemsha maji ya kunywa, kuosha matunda hili
kujikinga na magonjwa hayo.
Akuzungumzia mikakati waliojiwekea
katika kuhakikisha ulinzi na usalama katika kata hiyo aliesema tayali
ameshachukua hatua mbalimbali katika kuhakikisha swala la ulizi wa raia na mali
zao ni wa uhakika japo kumekuwepo na malalamiko hasa katika eneo la JIFTI
tayali ameshilikiana na polisi wa kituo cha kilwa road kuzuia ambushi
yakukamata watu wasiohusika badala yake kukamata wahusika wenyewe kwa
kutajiwa majina na kuwafwata majumbani kwao.
“Natoa wito kwa wazazi na walezi kuhakikisha wana
wakanya watoto wao wanaojihusisha na matukio hayo ya kiualifu kwani
watakua na ulinzi wa kiwango cha juu na hawatokubali lawama yoyote ile kutoka
kwa mzazi” Bw. Hashimu




