Manara: Mimi Ni Maarufu Kuliko Humprey Polepole

Afisa
habari wa klabu ya Simba, Haji Manara ameweka wazi kuwa yeye ni maarufu zaidi
nchini Tanzania kuliko Katibu wa Itikadi na Uenezi CCM, Humphrey Polepole.
Haji
Manara amesema kuwa yeye ni kada mzuri wa CCM na Polepole anafanya kazi kama
yake lakini hana jina kubwa kumzidi yeye kutokana na historia ya maisha yake na
chama hicho.
Manara
amedai kuwa CCM ndio chama kilichomsomesha nje ya nchi kuhusu masuala ya
propaganda na ameshawahi kuwa Katibu Mwenezi wa Mkoa wa Dar es salaam miaka ya
2007/10.
“Kwa
upande wa siasa mimi ni mwanachama wa CCM haswa, nilikuwa Katibu Mwenezi wa CCM
Mkoa wa Dar es salaam uongozi wangu ulikuwa 2007/10
"
Ilitokea tatizo ambalo ilibidi ifunguliwe kesi ya jinai kwangu, ilivyotokea
nikafikiri 2010 tunaelekea kwenye uchaguzi na mimi ni msemaji wa chama changu
cha CCM ndani ya Mkoa ndipo nikaamua kuandika barua ya kujiuzulu,“ameeleza Haji
Manara kwenye kipindi cha Kikaangoni cha EATV na kumtaja Polepole.
“Wote ni
Makada wa CCM ila mimi ni maarufu zaidi, sisemi kwa kudhihaki mimi na Humphrey
Polepole mimi maarufu, mimi ni kada wa Chama cha Mapinduzi na nimesomeshwa na
CCM kwa wachina, kuhusu Propaganda na nikikuambia hiki kikombe ni Kamera lazima
utakubali ,“amesema Haji Manara.



