Mwenyekiti Wa CCM Shina La JPM Kariakoo Hamisi Sadiki Amewataka Vijana Kujikita Katika Kufanya Kazi

Mwenyekiti Wa Shina
la JPM Kariakoo Bw. Hamisi Ahmedi Sadiki amewataka vijana kujikita zaidi katika
kufanya kazi pamoja na shughuli za kijamii kama kufanya usafi wa mazingira ili
kujiletea maendeleo badala ya kukaa vijiweni na kuendekeza starehe na matumizi
ya vilevi.
Akizungumza mapema
leo jijini dar es salaam mara baada ya kumalizika kwa mkutano wa vingozi wa Jumuhia
Ya Wazazi Wa Chama Cha Mapinduzi Ccm Mkoa Wa Dar Es Salaam alisema ya
changamoto ambayo imetajwa katika mkutano huo na naibu katibu mkuu wa chama
hicho taiofa ni kuwepo kwa vijana wengi ambao mda mwingi wanautumia kukaa
vijiweni na kutumia vilevi.
“kweli kumekuwepo
na wimbi la vijana kupenda kukaa vijiweni na kuendendekea matumizi ya pombe ili
sie tumelichukua kama changamoto na tunaenda lifanyia kazi kama vijana kwa
kuanza kuamasisha vijana wa kata yote JPM kuachana na fikra hizo na kujikita
katika kufanya kazi pamoja na usafi wa mazingira katika kata hiyo” alisema Bw. Sadiki.
Kwa kuanzia katika
kata yetu tayali tulisha andaa utaratibu wa kufanya usafi kila mwisho wa wiki na
kila mwisho wa mwezi kwa kushirikiana na viongozi wengine mbalimbali kuanzia
kata hili zoezi ilo kufanyika kwa ufanisi zaidi.
“shina la JPM
kariakoo lina wanachama zaidi ya 1700 hivyo sisi kama viongozi jukumu letu
kubwa ni kuhakikisha tunaendelea kutekeleza majukumu yetu kwa weredi hususani
katika swala la usafi wa mazingira” alisema.



