Wanachama 36 Kutoka Chadema na CUF Watimkia CCM Kata Ya Kilungule Jijini Dar.
Mwenyekiti Wa Tawi La Madukani Comrade Bw. Othumani
Mbonde akisoma majina ya wanachama wapya waliojiunga na chama hicho kushoto
kwake ni Mwenyekiti Wa Kata Hiyo Bi.Jeny Jerry wakati wa kukabidhi kadi za wanachama
wapya walioamia katika chama hicho jijini dar es salaam.
Na Sara Mlawas
Wanachama 36 kutoka chama cha demokrasia na
maendeleo (CHADEAMA) na chama cha wananchi (CUF) wamejivua uanachama na kujiunga
chama cha mapinduzi ccm katika tawi la maduka mawili lililopo kilungule jijini
dar es salaam.
Akizungumza jijini
Dar Es Salaam Mwenyekiti Wa Tawi La Madukani Comrade Bw. Othumani Mbonde alisema
kuwa kwa kufanya hafla fupi yenye lengo chanya kwa wana ccm imepelekea
wanachama wapya kutoka vyama pinzani na kujiunda chama cha ccm.
Alisema uzinduzi huu
wa ofisi ya tawi kwa ajili ya kuendesha shughuli za chama hivyo kuwasisitiza viongozi
wa ngazi mbalimbali na wanachama kukitumikia chama kwa dhati kwani chama
kinawadai.
Kwa upande wake Mwenyekiti
Wa Kata Hiyo Bi.Jeny Jery amewapongeza wanachama hao wapya walioamua kujiunga na
chama cha mapinduzi kitendo hicho wamedhilisha kuwa wanajitambua kwa kuhamia
chama kinachoongozwa na dola.
Alisema anaamini
wanachama hao waliorudi na kujiunga na chama hicho ambacho kinaongoza dola watahakikisha
wanashirikiana nao bega kwa bega kwa lengo la kutekeleza ilani ya chama.
Kwa upende wake mmoja
kati ya wanachama waliohamia chama hicho Bw. Saidi Jabili akizungumza kwa niaba
ya wenzake alisema jambo lililowashawishi kuhamia ccm ni kuunga mkono jitihada za
rais Magufuli ambazo amekuwa akuzichukua katika kutatua kero zinazowakabili
wananchi sambamba na kuhakikisha anaziba mianya ya rushwa pamoja na komesha ubadhilifu
wa aslimali za nchini.
“Natoa wito kwa wanachama wengene ambao bado
katika vyama vya upinzani kushirikiana na serikali ya awamu ya tano bega kwa
bega katika kuijenga Tanzania kwani wakati umefika wakuijenga kwani amepatika
kiongozi muadilifu na mzalendo wa kweli hivyo basi wanatakiwa kumpa ushirikiano
kutika kuleta maendeleo badala ya kuendekeza itikadi za kivyama” Alisema Bw Jabili.
Baadhi ya wanachama wapya waliojiunga na
chama cha mapinduzi ccm mara baada ya kukabidhiwa kadi za chama hicho jijini dar
es salaam.
Mwenyekiti Wa Tawi La Madukani Comrade Bw. Othumani
Mbonde akizungumza katika mkutano huo








