Rais Magufuli Ampa Milioni 100, Mgunduzi Wa Madini Ya Tanzanite

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli ameahidi kumpatia pesa kiasi cha Tsh.
Milioni 100, Mgunduzi wa Madini ya Tanzanite, mzee Jumanne Ngoma imsaidie
katika matibabu ya ugonjwa wake unaomsumbua wa kupooza.
magufuli amesema hayo leo, Aprili 6, 2018 katika eneo la Simanjiro ambako
anazindua Ukuta uliojengwa kuzungushiwa Migodi ya Tanzanite, Mirerani ili
kuzuia utoroshwaji wa madini hayo.
“Madini haya yalivumbuliwa na mzee Jumanne Ngoma mwaka 1967, na kupeleka
sampuli kwa Geologist (mtaalam wa miamba) kwenda kuyapima, pamoja na
kutambuliwa na Baba wa Taifa, Mwl Julius Kambarage Nyerere kwenye barua
aliyoisani Oktoba 8, 1980 akitambua kazi nzuri ya mzee Ngoma.
“Hata alipoyavumbua hakujua yatakuwa na thamani kubwa kiasi hicho, lakini
mzee Ngoma hakufaidika chochote, sasa naambiwa amepooza, nitampatia shilingi
milioni 100 zikamsaidie katika matibabu,” alisema Magufuli.



