NFRA Yajipanga Uzinduzi Wa Ujenzi Wa Maghala Na Vihenge Vya Kisasa Aprili 21, 2018
Kaimu Afisa Mtendaji
mkuu wa Wakala wa Taifa wa Hifadhi ya Chakula (NFRA) Bi Vumilia L. Zikankuba
akisisitiza jambo wakati akizungumza kwenye kikao cha kazi na wakuu wa idara,
vitengo na wafanyakazi wote wa NFRA Mkao makuu Mjini Dodoma, Leo 6 Aprili 2018.
Wakuu wa idara,
vitengo na wafanyakazi wote wa NFRA Mkao makuu Mjini Dodoma wakifatilia kwa
umakini kikao cha kazi kilichoongozwa na kaimu Afisa Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Taifa wa Hifadhi ya chakula (NFRA) Bi. Vumilia L. Zikankuba, leo 6 april 2018.
Kutoka kushoto ni
Meneja Rasilimali watu wa Wakala wa Taifa wa Hifadhi ya Chakula (NFRA) fredy Mbonde, Afisa Ugavi NFRA Magrethsalia Kavishe, na Mhandisi Imani Nzobonaliba ambaye ni mhandisi Mwandamizi NFRA wakifatilia kwa umakini kikao cha kaiz kilichofanyika katika ofisi za NFRA mtaa wa kizota Mjini Dodoma 6 April 2018.
Mhandisi Imani
Nzobonaliba ambaye ni Mhadisi Mwandamizi NFRA na Mratibu wa Mradi wa kuongeza uwezo na uhifadhi wa wakala wa taifa wa hifadhi ya chakula, akiwasilisha maelezo mafupi ya namna mradi utakavyotekelezwa wakati wa kikao kazi cha wakuu wa idara,vitengona wafanyakazi wote wa NFRA, leo 6 April 2018.
Kaimu Afisa Mtendaji mkuu
wa Wakala wa Taifa wa Hifadhi ya Chakula (NFRA) Bi Vumilia L. Zikankuba (Kulia)
akisisitiza jambo wakati akizungumza kwenye kikao cha kazi na wakuu wa idara,
vitengo na wafanyakazi wote wa NFRA Mkao makuu Mjini Dodoma, Mwingine pichani
ni Mkurugenzi wa maendeleo na Bishara wa Wakala wa Taifa wa Hifadhi ya
Chakula (NFRA) Ndg Mikalu Mapunda (Kshoto), Leo 6 Aprili 2018.
Na
Mathias Canal, NFRA-Dodoma
Waziri
Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe Kasim Majaliwa (Mb) anatarajiwa
kuwa mgeni rasmi kwenye sherehe za uwekaji wa jiwe la msingi kwa mradi wa
kuongeza uwezo wa uhifadhi wa wakala wa Taifa wa hifadhi ya chakula katika
dhifa itakayofanyika kwenye viwanja vya Ofisi za Wakala wa Taifa wa Hifadhi ya
Chakula zilizopo Mtaa wa Kizota Mjini Dodoma.
Hayo
yamebainishwa leo 6 Aprili 2018 na Kaimu Afisa Mtendaji mkuu wa Wakala wa Taifa
wa Hifadhi ya Chakula (NFRA) Bi Vumilia L. Zikankuba wakati akizungumza kwenye
kikao cha kazi na wakuu wa idara, vitengo na wafanyakazi wote wa NFRA Mkao
makuu Mjini Dodoma.
Bi
Zikankuba ameeleza kuwa Mradi huo utagharimu Dola za Kimarekani Milioni 55,
ikiwa ni mkopo wa masharti nafuu kutoka Serikali ya Poland ikiwa ni sehemu ya
kiasi cha milioni 110 kilichotolewa kwa serikali ya Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania.
Aidha,
amesisitiza kuwa mikataba ya ujenzi ilianza kufanya kazi tarehe 9 Disemba 2017
huku akisema Mradi huo utatekelezwa na kampuni mbili za Kandarasi kutoka Poland
ambazo ni (Feerum S.A na Unia Araj Realizacje Sp.o.o) ambapo msimamizi wa
utekelezaji wa mradi ni Wakala wa Majengo Tanzania (TBA).
Alisema
Mradi utahusisha ujenzi wa vihenge vya kisasa, maghala ya kisasa pamoja na
ukarabati wa ofisi na kutekelezwa katika maeneo nane ambayo ni Arusha (Babati),
Dodoma, Makambako, Mbozi, Shinyanga, Songea, Sumbawanga na Mpanda.
Baada
ya mradi kukamilika Wakala utakuwa umeongeza uwezo wa kuhifahi kwa 250,000 MT
zaidi (vihenge vya kisasa 190,000MT na maghala 60,000 MT) jambo ambalo litakuwa
chachu na mafanikio yenye tija katika kuunga mkono Juhudi za utendaji wa
serikali ya awamu ya tano inayoongozwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania Mhe. Dkt John Pombe Magufuli.
Alisema
kupatikana kwa Mradi huo nchini ni jitihada za Serikali ambazo zitapelekea
ukuaji wa uchumi nchini na kuchangia kuwezesha Tanzania ya viwanda ambapo kutawezesha
maghala ya Wakala kuweza kuhifadhi akiba ya Chakula ambayo itaendana na
mahitaji halisi ya dharura kulinganisha na ongezeko la watu nchini.
Hifadhi ya Chakula
inayohitajika kukidhi mahitaji ya dharula kwa miezi mitatu ni zaidi ya tani
500,000 ukilinganisha na tani 150,000 iliyokuwa inahitajika miaka ya 1992
Wakala ulipoanzishwa.
Pia, technologia ya
vihenge itawezesha Wakala kutumia teknolojia ya kisasa na hivyo kupunguza
gharama za uendeshaji, Itawezesha Wakala kuhifadhi chakula kwa muda mrefu Zaidi,
itasaidia kupunguza upotevu wa zao la mahindi baada ya kuvuna (posthaverst
loss) na kuongeza soko la mahindi nchini na kuimarisha usalama wa nafaka
inayohifadhiwa kwa kudhibiti sumukuvu (Aflatoxin) kwa mahindi
yaliyohifadhiwa.
Katika kikao kazi hicho Kaimu Afisa Mtendaji mkuu wa Wakala wa
Taifa wa Hifadhi ya Chakula (NFRA) Bi Vumilia L. Zikankuba amewasihi
wafanyakazi wote wa NFRA kufanya kazi kwa ushirikiano na kutambua kuwa nidhamu
na bidii yao itakuwa chachu ya mafanikio zaidi katika kuimarisha utendaji wa
NFRA.



