Simba Yaichapa Yanga 1-0 Uwanja Wa Taifa...Yanusa Ubingwa

Klabu ya soka ya Simba imeibuka na
ushindi wa bao 1-0 dhidi ya Yanga kwenye pambano la watani wa Jadi, lililopigwa
kwenye uwanja wa taifa jioni hii na kujiweka kwenye mazingira mazuri ya kutwaa
ubingwa.
Simba ambayo imeongoza ligi kwa muda
mrefu leo iliingia uwanjani ikipewa nafasi kubwa ya kushinda na pengine kwa
mabao mengi zaidi, lakini bao pekee la mlinzi mkongwe Erasto Nyoni dakika 37
limeamua mchezo.
Mazingira ya mabao hilo yalianzia kwa
Kevin Yondani kumchezea rafu Shomari Kapombe na kusababisha adhabu ndogo ambapo
mpira huo ulipigwa na Shiza Kichuya na kutua kichwani kwa Nyoni ambaye
aliutumbukiza nyavuni.

Baada ya ushindi huo Simba sasa
imefikisha alama 62 kwenye mechi 26 huku ikiwa haijapoteza mchezo hata mmoja
kwenye ligi kuu msimu huu. Sasa Simba inabakiza alama 5 pekee ili iweze kuwa
bingwa msimu huu.
Kwa upande mwingine kwenye mchezo wa
leo Yanga walilazimika kucheza pungufu kwa takribani kipindi chote cha pili
baada ya beki wa kulia Hassan Kessy kuoneshwa kadi nyekundu dakika ya 49
kutokana na rafu aliyomchezea Asante Kwasi.



