WADAU USALAMA BARABARANI WAPONGEZA KAULI YA RAIS MAGUFULI MATUKIO YA AJALI

Mkurgenzi
wa Chama cha Wanahabari Wanawake nchini (TAMWA), Bi. Edda Sanga kisoma tamko la
Mtandao wa Wadau wa Asasi
za kiraia unaotetea marekebisho ya sheria na sera ihusuyo usalama barabarani Tanzania
mapema leo 11 April 2018 jijini Dar es salaam.
Dar es salaam
Mtandao wa
Wadau wa Asasi za kiraia unaotetea marekebisho ya sheria na sera ihusuyo
usalama barabarani Tanzania, umempongeza Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa
Tanzania, Mhe. John Pombe Magufuli kwa kuguswa na kutoa maagizo mara kadhaa
kuhusu ajali za barabarani ambazo zimekuwa na athari nyingi kiuchumi na
kijamii.
Akisoma tamko la Asasi za kiraia mapema leo jijini
Dar es Salaam Mkurugenzi wa Chama cha Wanahabari Wanawake nchini (TAMWA), Bi.
Edda Sanga alisema ajali za barabarani zimekuwa zikisababishia madhara makubwa kwa
wananchi kama kupoteza Maisha, Ulemavu, Uharibifu Wa Mali pamoja na familia
nyingi zikiwa kubaki tegemezi baada ya kuondokewa na watu wanaowategemea.
“Mtandao Wa Asasi Za Kiraia unaunga mkono
kauli ya Rais aliyoitoa hivi karibuni ambapo alitoa maagizo kwa vyombo vya
usalama barabarani kufanya uchunguzi wa kina wa ajali iliyotokea katika kijiji
cha Makomero, Wilaya ya Igunga Mkoani Tabora Aprili 4, 2018. Ajali hiyo
ilitokea usiku na kusababisha vifo vya watu 12 baada ya basi la City Boy la
kutoka Karagwe kuelekea Dar es Salaam kugongana uso kwa uso na lori aina ya Fuso
lililokuwa linatoka Singida” alisema.
Ameyataja maagizo mengine ambayo mtandao huo unayaunga mkono ni kauli ya kulitaka Jeshi la Polisi, Kamati za ulinzi na Usalama za Mikoa na Wilaya na Mamlaka zote zinazohusika na usalama Barabarani kujitathimini, na kutafuta majawabu ya kwa nini ajali za barabarani zinaendelea kutokea kwa kusababishwa na uzembe na uvunjaji wa sheria za barabarani.

Afisa kutoka
Chama Cha Waandishi Wanawake (TAMWA) Bw. Edson Sosten akitoa ufafanua juu ya
hatua zinazochukuliwa na mtandao huo kudhibiti ajali za barabarani nchini
mapema leo 11 April 2018 jijini Dar es salaam.
Aidha Bi.Sanga aliongeza kuwa Pamoja na agizo
la Mheshimiwa Rais, la kuvitaka vyombo vya ulinzi na usalama barabarani na
mamlaka yake kutafuta majawabu kwa nini ajali zinaenaendelea kutokea nchini,
sisi kama mtandao wa Asasi za Kiraia kwa muda sasa tumekuwa pia tukijiuliza
swali kwa nini ajali za barabarani zimeendelea kutokea nchini?. Baada ya
tathimini na tafiti mbalimbali tulipata jawabu kwamba, kuna haja ya kufanyia
tena mapitio na kuboresha Sheria yetu ya Usalama Barabarani ya mwaka 1973.
Alisema sheria hiyo imejitahidi kwa kiasi
kikubwa kukabiliana na changamoto za usalama barabarani isipokuwa utafiti
uliofanyika unaonesha kuna mapungufu kadha wa kadha ambayo yanahitaji kufanyiwa
maboresho ili yaendane na hali ya sasa na pia iweze kukabiliana kikamilifu na
changamoto za ajali za barabarani pamoja na madhara yatokanayo na ajali hizo.
Alizitaja sheria ambayo wamependekeza
kufanyiwa kazi ni pamoja na; mwendokasi, matumizi ya mikanda, kofia ngumu,
matumizi ya vilevi na vizuizi vya watoto.
“Mwendokasi ndio unatajwa kuwa ndio chanzo
kikuu cha ajali- “the faster the speed the greater impact in the crush”.
Kifungu cha 51(8) cha Sheria yetu ya Usalama Barabarani ya mwaka 1973 inatamka
mwendokasi maeneo ya makazi ni 50km/h, kwa maeneo mengine utadhibitiwa na alama
za barabarani, na magari makubwa zaidi ya tani 3500 hayatazidisha 80km/h.
“Mapungufu ya sheria ni kwamba inatambua
maeneo machache katika kuzuia mwendokasi. Tunapendekeza kuwa sheria itamke
maeneo yote na si yale ya mjini tu/ makazi, itamke wazi kuhusu maeneo ya shule,
nyumba za ibada, maeneo ya michezo na mbuga za wanyama,” alisisitiza Bi. Sanga.



