JAFFO: Wazazi Hakikisheni Vijana Wenu Wanapata Elimu Ya Dini Ili Wawe Na Maadili

Dar
es salaam.
WAZIRI
Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (Tamisemi) Seleman Jaffo
amewataka wazazi kuhakikisha vijana wao wanapata elimu ya Dini itakayowasaidia
kukua na kuishi katika maadili.
Kauli
hiyo ameitoa leo jijini Dar es Salaam alipokuwa akizungumza kwa niaba ya Waziri
Mkuu Kassim Majaliwa katika Fainali ya Mashindano ya kuhifadhi Qur’an Tukufu ya
Afrika Mashariki inayoandaliwa na Taasisi Almanahilul Irfan Islamic Centre.
“Niwasishii
wazazi waendelee kuwapatia elimu ya dini vijana ili kupata maadili
yatakayowaongoza, kila mtu ahakikishe na atambue kuwa ni wajibu wake
kuhakikisha kijana wake anakuwa na maadili,” amesema Jaffo.
Amesena
kama watalelewa katika maadili hawataweza kushawishiwa kuvuruga
amana ya nchi na badala yake watawajibika kuilinda na aliwapongeza wazaizi kwa
kuwawizesha vijana kujifunza Qur’an.
Kwa
Upande wake Makamu wa Rais Mstaafu wa Awamu ya Nne Dk. Mohamed Gharib Bilal,
amewataka viongozi wa Dini kuendelea kuhamasisha vijana kusoma Qur’an.

Sheikh
Mkuu wa Dar es Salaam Alhad Mussa amesema lengo la kuhifadhisha Qur’an kwa
vijana ni kutaka kuwafanya waishi kwa kuakisi tabia ya Qur’an kama ilivyokuwa
kwa Mtume Muhammad (s.a.w).
“Hii
inasaidia kutengeneza vijana wenye maadili na wasio sumbua nchi, kijana
anayehifadhi Qur’an atakuwa ni kijana mwenye madili na kioo,” amesema Sheikh
Mussa.
Amesema
mwaka ujao shindano hilo litaanzia katika nganzi ya kitaifa, Afrika Mashariki,
Afrika na katika ngazi ya kimataifa.


Mkuu
wa Mkoa wa Mjini Magharibi, Zanzibar, Ayoub Mohammed Mahmoud amesema
shindano hilo linalenga kuendeleza Uislamu na umoja na aliwataka vijana wote
walioshiriki katika shindano kuyatumia vizuri mafunzo waliyopata.
Aidha
aliomba shindano hilo kutumika katika kuimarisha muungano. Lakini pia aliwataka
wananchi wasio waislamu kwa kipindi hiki cha mfungo wa ramadhan kuwa
na subra ili kulinda amani.


Naye
mlezi wa taasisi hiyo aliyekuwa Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi Dk.
Shukuru Kawambwa akitoa shukurani ametoa wito kwa taasisi nyingine kujitokeza
katika kusaidia mashindano kama hayo.
Kwa
upande wa shindano, lilikuwa na makundi manne ambayo ni ya Juzuu 10, Juzuu 20,
Juzuu 3 na Juzuu 30 ambapo mshindi wa kwanza ni Abubakar Mohammed Omar-Tanzania
Bara, wapili ni Amanya Adilu Ally-Uganda na watatu ni Suleman Ally
Matano-Kenya.



