Kesi Ya Mogogro Wa Ardhi kati Ya AG Kilangi Na Wananchi Wa Vicheji Kusikilizwa Julai 26
Mwanasheria Mkuu wa Serikali (AG), Adelardus Kilangi
Na Hussein
Ndubikile, Pwani
Baraza la Ardhi na Nyumba la
Halmashauri ya Wilaya ya Mkuranga Mkoa wa Pwani limesema Julai 26 mwaka
huu litaanza kuisikiliza kesi ya msingi ya mgogoro wa ardhi kati
ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali (AG), Adelardus Kilangi ambaye ni
mdai dhidi ya wadaiwa zaidi ya 70 ambao ni wananchi wa Kijiji cha Vicheji
kilichopo wilayani humo.
Hatua hiyo imdikiwa jana wakati Mwenyekiti wa
baraza hilo Mwakibuja alipokuwa akisoma uamuzi wa mapingamizi yaliyowasilishwa
na pande mbili katika shauri hilo.
Akisoma uamuzi huo leo wialyani humo,
Mwenyekiti Mwakibuja aliitupilia mbali hoja ya mdai Kilangi ambayo
iliwasilishwa kwa maandishi barazani hapo kupitia wakili wake Daudi Maginge
Kuwa wadaiwa hawana nguvu ya kumshtaki..
" Baraza linatupilia mbali hoja hiyo kwa
kuwa kila raia ana haki ya kushtaki na kushtakiwa,' Anadai Mwenyekiti
Mwakibuja.
Pande mbili zilwasilisha mapingamizi
mbalimbali kwa maandishi huku wadaiwa wakiliomba baraza limuongeze mwenyekiti
wao wa kijiji Ramadhani Maulid katika shauri hilo ombi ambalo lilitupiliwa
mbali kwa kukosekana vielelezo vya kutosha.
Mgogoro katika kesi namba 55 ya mwaka 2016
unawahusisha wadaiwa Said Kaisi 46, Bakari Saguti 60, Omary Issa 42, Juma Omary
40, Salima Bilali (53), Regia Issaya(55) ,Sada Abdallah(72) na ambao
kwa pamoja wanadaiwa kuingia kwenye shamba la Kilangi bila kibali.
Washitakiwa hao kwa pamoja inadaiwa kuwa Mei
9 2016 katika Kijiji cha Vicheji waliharibu Miti 13 ya Minazi na nyumba mbili
vyenye thamani ya Sh. Mil 22.2 mali ya AG Kilangi.
Kesi hiyo imeahirishwa hadi julai 26 mwaka
huu itakapokuja kwa ajili ya kuanza kusikilizwa ambapo nje ya mahakama wadaiwa
waliulalamikia uongozi wa baraza hilo kwa kuwachanganya haswa
pale muda wa kesi kuanza tofauti ilivyopangwa awali.
Akizungumzia suala la muda kwenda tofauti
mdaiwa Saidi Kaisi amesema baraza limekuwa likipangua muda wa kesi yao bila
taarifa hali inayowanyong'onyeza na kuwafanya wajiulize maswali mengi kuhusiana
na mwenendo mzima wa kesi.
" Tunafahamu kuw kesi yetu tunapambana
na mtu mkubwa serikalini lakini kwakuwa serikali yetu ni sikivu tunaimani
mahakama itatenda haki,'amesema kaisi
Naye Jonas Kyando ambaye ni mdaiwa
amebainisha awali waliambiwa kesi hiyo ingsikilizwa muda wa saa 5 asubuhi
lakini cha kushangaza saa 4 asubuhi uamuzi ulitoka bila kuambiwa hali
inayowaweka njia panda kupata haki yao.
Hata hivyo wanakijiji wengine
waliungana kma pamoja kuomba haki ya wanyonge isidhulumiwe



