Maonyesho Ya Bunge Property Expo Yawa Kivutio Dodoma

Kampuni ya Terranova imeandaa
maonyesho ya milki kuu , nyumba na nyenzo za ujenzi katika viwanja vya bunge
jijini Dodoma.
Maonyesho hayo yamezinduliwa rasmi
jana na Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi mheshimiwa William
Lukuvi.
Akizungumza wakati wa uzinduzi
huo,Waziri Lukuvi aliupongeza uongozi wa Kampuni ya kizalendo
inayoongozwa na vijana waliopata elimu katika vyuo vikuu vya hapa nchini
kufikisha elimu kuhusiana na sekta nzima ya ardhi na kuiletea Tanzania mendeleo
kutokana na rasilimali.
Aidha alitoa rai kwa wadau kulipa
kodi halali katika uendeshaji wa shughuli zao ili kwenda sawa na kasi ya ukuaji
kiuchumi kupitia mapato ya ndani.
"Sisi tumeanza na tutazidi
kuhamasisha wawekezaji wafike Dodoma , ili adhma kuu ya serikali ya kuhamia
Makao makuu ya nchi izidi kupata tija kwa maendeleo yetu" ,alisema
mkurugenzi mkuu wa kampuni ya Terranova Emil Sylvester.
Wadau mbalimbali wamejitokeza
kuonyesha bidhaa mbalimbali katika sekta hiyo wakiwemo, Nabaki Afrika, Fumba
developments, Ngorongoro conservativation, Alrais developers na taasisi ya
mwanamke ardhi.











