Meya JACOB: Vijana Halmashauri Ya Ubungo Jitokezeni Kuchangamkia Fursa Mikopo Kutoka Kwenye Mfuko Wa Fedha Wa Maendeleo.

Meya Wa Ubungo Jijini Dar Es Salaam, Mhe. BONIPHACE JACOB.
Na Semtawa Jafari
VIKUNDI vya vijana
katika Halmashauri mpya Ubungo vimetakiwa kuchangamkia fursa ya mikopo kutoka
kwenye mfuko wa fedha wa maendeleo, zilozotengwa kwa ajili ya vijana na
wanawake katika wilaya hiyo.
Akiongea katika
kipindi cha cha Joto la Asubuhi kinachorushwa na E. FM, Meya Wa Ubungo Jijini Dar
Es Salaam, Mhe. BONIPHACE JACOB, alisema hadi sasa mwamko wa vijana katika
kuomba mikopo hiyo ni mdogo ukilinganisha na wanawake.
"Wanawake
wapatao 2000 wamejitokeza, kuchukua mkopo na wamekuwa wakifanya shughuli za
ujasiriamali mfano biashara ndogo ndogo na wengine kujianzishia viwanda vidogo
kama vile kutengeza sabuni, batiki na nyingine," alisema Mhe. Jacob.
Alisema ameamua
kuwaamasisha vijana baada ya kutoridhishwa na kasi ya vijana ya kwenda kuomba
mkopo wakati fedha zipo kwa ajili yao ambazo zimetengwa ziwasaidie katika kuwaletea
maendeleo yao.
“Ofisi yaku na ile
ya maendeleo zimekuwa zikiwanahamasisha vijana wa wilaya hiyo kwenda kuchukuwa
mkopo kwa sababu wametengewa kiasi cha sh. Bil. 1.9 ambazo zimekusanywa kutoka
kwenye vyanzo vya kodi zao, natoe rai kwa vijana kuondokana na mawazo ya kwamba
lazima wanapokwenda kuomba mkopo lazima watahitajika kuwa labda na dhamana ya
nyumba wakati kitu kamahicho katika mikopo hiyo ya halmashauri hakipo” ”Alisema
Mhe. Jacob.
Aidha Mhe. Jacob
aliongeza kuwa mikopo inyotolewa na Halmashauri hiyo riba yake ni ndogo huku
akifafanua kuwa kwa mwenye kukopa sh. Mil. 1; riba yake ni sh. 80,000 ambayo
anaamini kwa mjasiriamali mwenye nia ya dhati anaimudu.
Alitaja mashariti
ya mkopo huo kuwa lazima waombaji wawe kwenye kikundi cha kuanzia watu watano
huku wakiwa na andiko linaloonesha mchanganuo wa biashara zao.
Alisema baada ya
hatua hiyo itabidi waende kwa Mtendaji Kata kwa ajili ya usajili, baada ya
usajili huo, kisha wazo lao hilo litahakikiwa na maofisa maendeleo wa wilaya
ili kujiridhisha kama kikundi husika kimekidhi vigezo.
"Nimekuwa
mstari wa mbele kuwahamasisha vijana hadi nimefikia hatua ya kuimba wimbo ambao
unahamasisha vijana, wanawake na wale waliokata tamaa wajitokeze kuomba mikopo
hiyo Alisema Jacob.
Pia Mhe. Jacob
alimetoa ufafanuzi Kuhusu wananchi wanaodai fidia baada ya kupisha bomba la
gesi, alisema suala hilo limekwama kwa vile serikali kwa sasa haina fedha za
kuwalipa huku akisisitiza kuwa suala hilo kwa sasa liko wizarani.



